Ahmed Alahmar akisema kwa timu ya vijana ya kitaifa : mmeheshimu Misri.

Ahmed Alahmar, mchezaji maarufu wa klabu ya Zamalek na timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa mikono amepongeza timu ya vijana ya kitaifa baada ya ushindi wake kwa michuano ya kombe la dunia, ambapo timu ya kitaifa hiyo imeshinda dhidi ya timu ya kitaifa ya Ujerumani katika mechi ya fainali 32- 28.

 

Alahmar amezungumza katika matangazo ya runinga kupitia idhaa ya  "Time Sport" : wachezaji wa timu ya vijana kwenye kiwango cha juu na kitu cha heshima baada ya kushinda kwao kwa michuano ya kombe la dunia kwa vijana.

Akiongeza : wachezaji wamekuwa wanajua sana kiasi cha jukumu kilichowekwa juu yao, na wameweza kuheshimu kwa Misri.

 

Ameongeza kusema kuwa timu ya kitaifa imefuzu kwa idadi kubwa ya magoli, na hii sio jambo sahili katika mpira wa mikono.

 

Pia amesema kuwa wachezaji hao watakuwa msingi kwa timu ya kitaifa ya kwanza katika michuano ya kombe la  dunia itakayofanyika nchini Misri, mwaka wa 2020, ambayo itakuwa lengo letu kuu ni kufuzu kwa michuano hiyo.

Comments