Baraza la mawaziri lapongeza timu ya mpira wa mikono ya Misri kwa kufanikiwa kushinda kombe la dunia.
- 2019-08-19 11:56:45
Baraza la mawaziri
limetoa pongezi kubwa kwa timu ya mpira wa mikono ya Misri kwa mnasaba wa
kushinda kombe la dunia likieleza kuwa
serikali ya Misri imefurahishwa sana kwa umahiri mkubwa ulioneshwa na timu hiyo
kwenye mashindano ya michuano hii hadi kupata ushindi hatimaye. Pamoja na hayo, limewapongeza makapteni kwa
juhudi zao kubwa walizozifanya.
Wakati huo huo, Baraza
la Mawaziri limesisitiza kuwa ushindi huu (kupata taji) linatukumbusha tena kwa
utashi wa vijana wamisri na nguvu yake isiyo na mipaka ya kupata ushindi kwenye
michuano, pamoja na kutimiza mafanikio katika nyanja mbalimbali kwa uamuzi na
uvumilivu wote ambao tunapaswa kuwa nao.
Aidha, Baraza la
Mawaziri limewahimiza wale wanaowakilisha nchi yao katika sekta mbalimbali
likisema kuwa, wanapaswa kuwa na umahiri wa kitu wanachokifanya, pamoja na
kutia bidii zao zote ili kuinua jina la Misri juu kwenye makongamano mbalimbali
ya kimataifa.
Comments