Katika
muktadha wa mfululizo wa shughuli na mipango inayotolewa na Azhar Shariif katika kuadhimisha ofisi ya raisi wa Misri
kwa umoja wa kiafrika katika mwaka 2019. Na katika muktadha wa mapendekezo na
mielekeo ya imamu mkuu, DK, Ahmed EL-Tayb ambaye ni shekhe wa Azhar Shariif kwa
dharura ya kuwekeza na kutumia vifaa vyote vya uchukuzi wa Azhar barani Afrika
kwa ajili ya kuendana na harakati za Misri kwa ajili ya bara la Afrika. Wakati
ambapo chuo kikuu cha Azhar kimetangaza katikati ya vifijo na nderemo ya
kiupendo, chuo kikuu cha Azhar kimetangaza ushiriki wa mkubwa wa kimisri na wa
kiafrika katika ufunguzi wa makao ya kikanda ya kudumu ya umoja wa vyuo vikuu
vya kaskazini mwa Afrika. Na hayo yamehudhuriwa na DK. Ahmed EL-tayb, shekhe wa
Azhar Shariif na DK. Mohamed Mukhtar Juma, waziri wa wakfu na DK . Shawki
Alaam, mufti wa jamhuri ya kiarabu ya kimisri na DK.Mohamed Hussen EL-Mahrusi,
mkuu wa chuo kikuu cha Azhar na DK. Aurland Antonion, mkuu wa umoja wa vyuo
vikuu vya kiafrika na DK.Aitian Ahili, katibu mkuu wa umoja wa vyuo vikuu vya
kiafrika ukiongezea na baadhi ya mawaziri na mabalozi kutoka mataifa mbali
mbali barani Afrika. Mkutano huu
umeanzia utoaji wa maonesho ya ustaarabu wa Misri na Azhar Shariif
ikishirikiana na kituo cha
kuhifadhi kumbukumbu za urithi katika
maktaba ya Alexandria. Kisha mkuu wa
chuo kikuu cha Azhar, DK. Mohamed EL-Mahrusi amewataka wote kusimama kwa muda wa dakika moja kuomboleza
vifo vya wahanga wa ndege ya Ethiopia iliyoanguka siku ya juma tatu iliyopita. Kisha
ameashiria kwamba taasisi ya Azhar Shariif imeendelea kuwa juu tangu ilipoanzishwa na mpaka sasa kutokana na kulinda kwake mfumo wa ukati licha ya kuanguka kwa mataifa na nidhamu
pamoja na taasisi. Na ameongeza kwa kusema
kwamba Azhar Shariif sio tu taasisi ya kikanda bali ni taasisi ya
kimataifa ambayo ndani yake wanajifunza kutoka mataifa takriban 100 ulimwenguni
kote.
Ilhali
waziri wa elimu ya juu,DK.Khaled Abdal Ghafar
amesisitiza kwamba ufunguzi wa makao ya kikanda ya umoja wa vyuo
vikuu vya kiafrika ya kaskazini mwa Afrika yaliyopo chini ya chuo kikuu cha Azhar
unazingatiwa kuwa ni hatua muhimu sana kwa ajili ya kuendana na matokeo kadhaa
na mabadiliko ya kijamii na ya kiuchumi na ya kisiasa ambayo bara letu na dunia
zinakabiliana nayo. Na yanayotulazimisha
tuhangaikie kwa ajili ya kuimarisha juhudi za pamoja kwa ajili ya kuleta
maendeleo ya kibinadamu ukiongezea na
kuboresha viwango vya uwezo na
umahiri wa kibinadamu kwa kuanzia kwenye
imani kwamba mwanadamu ndiye upeo na lengo
kwa maendeleo na uboreshaji unaoshuhudiwa na mataifa na jamii.
Ilhali katibu mkuu wa umoja wa vyuo vikuu vya
kiafrika, DK. Aition Ahili ameashiria
kwamba kuaznzisha kwa ofisi ya kikanda
kwa ajili ya umoja wa vyuo vikuu vya kiafrika nchini Misri kunazingatiwa kuwa ni mwanzo wenye nguvu na njia sahihi kwa ajili
ya kukidhi mahitaji ya elimu ya juu barani Afrika na Misri ukiongezea na kuziba
pengo na kupunguza unyonge katika nchi nyingine. VileVile inazingatiwa kuwa ni
fursa kwa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kukabiliana na changamoto kadhaa
zinazokumbana na umoja huu. Akiashiria kwamba
vyuo vikuu vya kiafrika vinahangaikia kuanzisha makao ya kikanda katika mataifa yote ya
kiafrika. Jambo ambalo linazingatiwa kuwa ni hatua ya pili kwa ajili ya kuhakikisha mikakati ya elimu ya
juu ya kibara katika mwaka 2025 ukiongezea na
hatua hiyo inafanya kazi juu ya kuunganisha juhudi kwa ajili ya kusaidia
elimu na teknolojia. Kama pia Ahili
amempelekea raisi EL-Sisi pongezi
zake katika kuadhimisha ofisi ya raisi
wa Misri kwa umoja wa kiafrika
akasifu mchango mkubwa unaotolewa na chuo kikuu cha Azhar kwa ngazi ya kiafrika kutoka katika kiwango
cha kipekee katika orodha ya kiafrika.
Kwa
upande wake balozi, Abdal Hamiid Abu
Zahar,mkuu wa ujumbe wa kudumu wa umoja wa kiafrika wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu
ametoa shukurani yake kwa taasisi ya Azhar
Shariif kwa ajili ya misaada yake kwa maelfu ya wanafunzi wa kiafrika wanasoma
katika chuo kikuu cha Azhar ukiongezea
na juhudi zake katika kueneza uislamu wa ukati wenye kuangaza katika dunia
ambayo uislamu unakabiliwa na upotoshaji
wa aina mbali mbali wenye lengo. Akiashiria kwamba uandaaji wa Misri kwa tukio
hili lililo muhimu unazingatiwa kuwa
ni dalili bora zaidi kwa kuwajibika kwa
kuzingatia zaidi upeo wa kiafrika.
Aidhaa tukio hilo linazingatiwa kuwa
ni mpango mzuri na habari njema kwa ajili
ya wanafunzi wa kiafrika. Ambapo chuo kikuu cha Azhar kikawa upande unaopendwa sana na wanafunzi wa
kiafrika. Akisisitiza kwamba
tunalazimishwa kuboresha kiwango cha vyuo vikuu vya kiafrika kutokana na
kuendana na mabadiliko mapya zaidi ya
kisayansi na ya kimaarifa ukiongezea na
upanuzi wa mchango wa umoja wa vyuo vikuu vya kiafrika kutokana na kuyasaidia
mataifa ya kiafrika kwa ajili ya kufikia kiwango cha upekee ambacho
tunakitazamia.
DK.
Ahmed EL-tayb katika hotuba yake amesisitiza msaada ya raisi Abdal Fatah
EL-sisi kwa ajili ya uandaaji wa Misri kwa makao ya kikanda ya umoja wa vyuo
vikuu vya kaskazini mwa Afrika. Akiashiria kwamba hayo yanazingatiwa kuwa ni
tukio la kihistoria linakuja katika muktadha wa kuthibitisha mahusiano ya kina
ya kimikakati na uwazi wake sio tu barani Afrika bali ni ulimwenguni kote. Akisisitiza kwamba Misri
inazingatiwa kuwa ni nchi inayoandaliwa
kwa ajili ya kuibeba risala ya umoja wa vyuo vikuu vya kiafrika pamoja
na kuifikisha risala hiyo kwa mabara yote ya ulimwengu.
Na
imamu mkuu ameongeza kwa kusema mchango wa Misri katika kuyaeneza maadili ya
kuvumiliana na amani na khasa pamoja na hatua zake zenye kuharakisha kwa ajili
ya kumaliza ugaidi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kudumu ul ukiongezea na
kuti kutosheleza maisha bora kwa raia.
Jambo ambalo litakuwa na matokeo makubwa
kwa raia wa bara jeusi. Na
hayo kutokana na Misri inayozingatiwa kuwa ni mlangpo wa kaskazini
mashariki mwa bara la Afrika. Akiashiria
kwamba chuo kikuu cha Azhar kinajumuisha
zaidi ya wanafunzi wa kike na wa kiume elfu 6 kutoka Afrika ukiongezaea na chuo kikuu hiki kinatosheleza nafasi za
masomo kwa ajili ya wanafunzi wa kike na wa kiume elfu2. Aidhaa ametangaza kwamba katika mwaka
huu kutatimia kufungua kitengo cha kisayansi kwa masomo ya
upili kwa wanafunzi wa kiafrika
katika chuo cha tafiti za kiislamu kwa ajili ya kuwaandaa wananchi wa kiafrika
kwa kusaidia katika kuhakikisha malengo ya maendeleo barani Afrika. VileVile imamu mkuu amewasifu vijana wa kiafrika akisema " vijana wa
kiafrika katika mataifa yote ya Afrika . Hakika maendeleo ya bara lenu lililo tajiri
kwa rasilimali zake za kimaumbile na za kibinadamu hayawezi kupatikana
isipokuwa kwa akili zenu na mikono yenu nyinyi wenyewe sio wengine".
Comments