Timu 24 za wakazi wa kiafrika zinashiriki katika mfano simulizi wa mashindano ya Afrika
- 2019-04-05 13:04:54
Wizara ya vijana na michezo chini ya uangalizi wa
DK. Ashraf Sobhy, imetangaza ushiriki wa vijana wa wakazi wa kiafrika
nchini Misri kwa mataifa yaliyofuzu kwa michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika kwa
mwaka 2019 katika utekelezaji wa mfano simulizi wa mashindano ambao
unatekelezwa na wizara hiyo katika kipindi kutoka 19 April hadi 26 April katika
uwanja wa kituo cha vijana wa kisiwa.
Na hayo yanakuja katika muktadha wa maandalizi
wa Jamhuri ya kiarabu ya kimisri kwa ajili ya uandaaji wa michuano ya kombe la
mataifa ya kiafrika katika mwaka huu. Na
katika muktadha wa ofisi ya raisi wa Misri kwa umoja wa kiafrika na kama ni uthibitisho wa mchango iliyo muhimu wa michezo kwa kuzingatia kuwa ni nguvu iliyolala ambayo
inatoa mchango wa kuwaweka pamoja
wananchi wa mataifa mbali mbali. VileVile timu za taifa zilikwishapangwa
kabla ya kura ya michuano ya Afrika. Nafasi
ya kwanza katika orodha inajumuisha
timu za Tunisia, Ghana, Misri, Sengali, Kameruni na Evary Coast. Nafasi ya pili katika orodha inajumuisha timu
za Moroko, Nigeria, Kongo, Mali, Aljeria na Gini. Nafasi ya tatu katika orodha inajumuisha timu za Uganda, Gini Bisau,
Afrika ya kusini, Zimbabwe, Angola na Moritania. Nafasi ya nne katika orodha
inajumuisha timu za Benini, Burundi, Tanzania, Nambia, Kenya na Madagaska.
Mfano
huu unalenga kuendeleza na kuimarisha mahusiano baina ya wakazi wa kiafrika
nchini Misri na wizara ya vijana na michezo. Ukiongezea na ujenzi wa moyo
chanya huonekana katika njia ya kushangilia mashindano makubwa katika Juni
ijayo. Inafaa kusema kwamba umoja wa kiafrika wa mpira wa miguu (KAF)
umeianisha miadi ya kupiga kura kwa ajili ya kura ya mashindano ya Afrika
katika 12 April ijayo. Na patatumika kura ile ile katika mfano simulizi wa
mashindano ya Afrika.
Comments