Waziri wa vijana na michezo anawapokea mabingwa wa mpira wa mikono katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kairo.
- 2019-08-21 12:53:54
Alfajiri ya
jana, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo ameipokea timu ya kitaifa
ya Misri ya mpira wa mikono na ambayo imeshinda michuano ya dunia kwa vijana
iliyofanyika nchini Macedonia, mnamo kipindi cha tarehe 6 hadi 18 Agosti.
Mapokezi yameshuhudia
kuhudhuria kwa mhandisi (Hisham Nasr)" mwenyekiti wa Muungano wa Kimisri
wa mpira wa mikono', pia mahudhurio ya wanachama wa baraza la uongozi la
Muungano wa mpira wa mikono na umati wa watu wengi.
Sobhy
ameelezea furaha yake kubwa kwa ushindi huo ambao inaonyesha mabadiliko ya
taratibu kwa michezo ya mpira wa mikono, mpaka imefikia kilele kwa kuchukua
kwake nafasi ya kipekee kwa michezo hiyo kwenye ngazi ya kimataifa katika umri
wa vijana.
Waziri wa
vijana na michezo ametoa pongezi kwa rais Abd Alfatah Elsisi, ambaye ni rais wa
Jamhuri ya Misri na msaidizi wa vijana wa Misri katika michezo mbalimbali,
akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa una imani kubwa kuwa michezo ni usalama wa
kitaifa na mojawapo ya nyanja muhimu zaidi zinazosaidia katika muundo wa
utamaduni wa jamii na kuchangia kufanikisha maendeleo kamili, akiashiria kuwa
mkakati wa wizara ya vijana na michezo na yanayochukulia mkakati wa ujenzi wa
kibinadamu na maono ya Misri 2030 umesisitizia mipango ya kipekee ya serikali
chini ya uongozi wa Dokta Mostafa Madbuli ambayo inalenga uandaaji wa vizazi
katika michezo mbalimbali kwa ajili ya vinakuwa nguzo kuu za baadaye kwa timu
za kitaifa inayolenga kugundua wachezaji wa kipekee katika michezo mbalimbali
ikiwa ni binafsi au pamoja.
Waziri wa
vijana na michezo amesifu mfumo wa mpira wa mikono kwa mfumo kamili na
unaofanya kulingana na mkakati wazi unalenga kwa uandaaji wa vizazi vya kipekee
katika michezo hiyo, hutegemea kazi ya kudumu na inayoendelea wakati wa upanuzi
wa msingi wa mashindano, na kupata kwa wachezaji kwa ajili ya kuandaa kwao ili
kuwa msingi wa timu za kitaifa kwa umri zake mbalimbali.
Dokta Ashraf
Sobhy amemaliza kuwa wizara haichelewi kwa kutoa misaada kwa mabingwa wa dunia
katika mpira wa mikono, akisisitiza kuwa Ufadhili utakaolipwa utakuwa stahiki
kwa ushindi uliyofanywa.
inatajwa kuwa
timu yetu ya kitaifa imeanza mechi zake katika michuano hiyo kwa kufuzu dhidi
ya mwenzake, timu ya kitaifa ya Sweden kwa tija 32-29, kabla ya kushindwa kwake
toka timu ya kitaifa ya Ufaransa kwa tija 28-32, kisha imeshinda timu ya
kitaifa ya Taiwan kwa tija 36-25.
Comments