Balozi wa Tanzania nchini Misri ameshukuru chuo kikuu cha Alexandria

Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa Suleiman Nassor ameelezea shukrani zake kwa Chuo Kikuu cha Alexandria juu ya duru inayochezwa na Chuo hicho kwa kuandaa msafara wa matibabu kwenda Tanzania mapema mwezi huu wa nane tulionao, kwa kushirikiana na mawakala na taasisi za afya kwa ajili ya maendeleo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, pamoja na ushirikiano wa Jumuia inayoshughulikia maradhi ya watoto yanayohitajia upasuaji katika hospitali ya Al Shatbiy ya Chuo Kikuu, ambapo msafara huo wa madaktari ulitoa huduma zake za kimatibabu ndani ya siku tano.
Balozi Issa ameongezea kusema kwamba shughuli hizo zinaakisi duru muhimu ya Misri katika mchango wake barani Afrika, hususani nchi za bonde la mto wa Nile. 


Comments