Kwa mara ya kwanza .. Kituo cha kufundisha lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kairo.

 Lengo la Kituo hicho ni Kuunga mkono Siasa za kimisri kuelekea bara la Afrika.

Kitivo cha masomo ya juu ya kiafrika , moja wapo ya vitivo vya Chuo Kikuu cha Kairo, imetangaza kuanzishwa kwa kituo cha kwanza kilicho maalum katika kufundisha lugha za Kiafrika katika chuo kikuu, Kwa hivyo  katika mraba wa hatua na juhudi za chuo hicho, kuhuduma na kuunga mkono siasa za kimisri zinazoongozwa na Rais Abdel Fattah al-Sisi, Inalenga kufungua Afrika na kuunganisha mahusiano yote na nchi za Kiafrika na watu, Kulingana na maono ya Chuo Kikuu cha Kairo, kinachoongozwa na Dokta Mohamed Othman El-Khesht, Ili kuajiri sayansi na utafiti wa kisayansi, kuhuduma maswala ya Misri na nchi zote za Kiafrika.


Katika suala hili, Dokta Mohamed Nofal, Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya juu  ya Kiafrika, alisema kwamba kuanzishwa kwa kituo hicho kunakuja kwa imani juu ya umuhimu wa suala la Kiafrika, na umuhimu wa kulizingatia kwa pande zake zote , hasa mwelekeo wa kitaaluma  kitamaduni, na kilugha .

Noufal alisema kuwa kituo hicho kitafundisha lugha kuu za Kiafrika zinazoenea katika bara lote kama vile: Kiswahili, Kihausa, Kiamhariki na nyingine , kwa wanafunzi na wale wanaopenda kujifunza lugha za Kiafrika,Kituo hicho Lengo lake ni aina  zote za jamii ya kimisri na vile vile ndugu waafrika wanaopo nchini  Misri.

Mkuu wa masomo ya kifrika  aliongeza kuwa kituo hicho kitatoa huduma ya kufundisha lugha za Kiafrika kwa wasiozitamka , tafsiri kutoka lugha za Kiafrika kwa Kiarabu na kinyume chake, na utafsiri wa cheti, hati, masomo na utafiti kutoka na  kwa lugha za Kiafrika linalosaidia wanafunzi, watafiti na sehemu zote za jamii.

Nofal alihitimisha kauli yake kwa  kuwa huduma za kituo hicho, shughuli, kozi na tafsiri zitatangazwa katika siku chache zijazo, akisisitiza juu ya  uangalifu wa Kitivo cha masomo ya juu ya kiafrika , Chuo Kikuu cha Kairo kutekeleza mtazamo na mielekeo ya kimisri chini na kufikia uongofu na ukamilifu wa kimisri kiafrika  katika nyanja mbali mbali.


Comments