Kuimarisha kitambulisho cha Misri .. Mkutano katika Wizara ya Vijana na Michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma/kiserikali
- 2019-08-23 15:57:26
Wizara ya Vijana na Michezo, kupitia Idara kuu ya Programu za Kitamaduni na za kujitolea, iliandaa mkutano chini ya anwani ya "Kuimarisha Kitambulisho cha Misiri", ndani ya shughuli za mkutano wa wanafunzi wa vyuo vikuu chini ya kauli mbiu "Kujenga kwa Wahusika wa Wamisri", ambayo ilifanyika wakati wa kipindi cha tarehe 17 hadi 21 Agosti katika mji wa vijana wa Port Said
Semina hiyo iliwasilishwa na Dokta . Ramadan Korany,
mtaalamu wa maswala ya Kiafrika katika Taasisi kuu kwa ya Habari na Maarifa
(SIS) Alisisitiza kiburi cha Misiri kwa kitambulisho chake cha Kiafrika, na
kuashiria kwamba hiyo ilithibitishwa na vifungu vya Katiba ya Misri.
Mtalaamu wa Masuala ya Kiafrika katika Taasisi kuu kwa
Maarifa aliashiria kwa umuhimu wa jukumu
la sasa la Misri katika bara la Afrika kwa kuzingatia uwepo wa urais wa Misri
kwa Umoja wa Afrika, akizungumzia umuhimu wa jukumu la media, utamaduni na
elimu katika kukuza utambulisho wa Misiri ya Kiafrika hasa makundi ya wanafunzi na vijana.
Dokta . Ramadan Korany alizungumzia umuhimu wa Ajenda
ya 2063 kama kielelezo cha kazi ya
maendeleo ya Kiafrika, akiashiria umuhimu wa maoni ya kitamaduni na ya
wanafunzi katika kujenga kitambulisho cha Kiafrika kati ya vijana wamisri ,
mwishowe kwa faida ya masilahi ya Kimisri katika bara la Afrika kufaidika na
kukuza uhusiano wa Kimisri-Kiafrika
kulingana na kanuni ya (Faida Kwa Wote).
Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki 120 na unakuja katika
mraba wa mkakati wa Wizara ya Vijana na Michezo kuelekea kukuza na maendeleo ya
wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri katika nyanja zote, na kuambatana na mkakati
uliozinduliwa na Rais Abdel Fattah El Sisi kuelekea kumjenga mtu mmisri.
Comments