Timu ya kiolimpiki inaikabili Saudi Arabia ( kimataifa ) mnamo Septemba .

 Shirikisho la Soka la kimisri liliidhinisha mpango wa kuandaa timu mnamo mwezi wa septemba ujao wakati wa mkutano ambao umefanyiwa na naibu dokta Tharwat Soielm , mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la soka  na kapteni Shawki Gharib , mkurugenzi wa kiufundi wa timu .

 

Osama Esmail meneja wa vyombo vya habari vya timu  alieleza kwamba timu ya olimpiki itaikabili mwenzake  Saudi Arabia  tarehe 7 na 10 mnamo septemba katika michezo miwili ilipitishwa kimataifa na itafanyika ndani ya  Misiri , na sasa kuna mapendekezo ya kufanyika michezo hiyo nje ya  kairo baina ya  uwanja wa Esmaillia au wa Suez au wa Aleskandaria . 

 

Inayotarajiwa timu ya Saudi Arabia nzima itafika Kairo tarehe 5 mwezi wa Septemba baada ya kujiandaa kwa fainali za Asia inayostahili michezo ya olimpiki Tokyo 2020 , vilevile wafanyikazi  wa kufundisha  wa timu ya wamisri watatangaza orodha ya wachezaji  mwishoni mwa Agosti  ili kushiriki katika kambi inayofuata, ambayo itaanza mwanzoni mwa septemba na kuendelea hadi tarehe maalum ya mchezo wa pili .

 

Inatajwa kwamba kambi ya timu ya Misri ya olimpiki inakuja kwenye programu ya kuandaa timu kwa ajili ya kushiriki katika fainali za mataifa ya kiafrika chini ya miaka 23 , yanayopangwa na Misri katika kipindi cha 8 _22  Novemba ijayo , na wakati huo huo , inastahili michezo ya olimpiki .

Comments