Misri inashinda juu ya Japan katika michuano ya dunia kwa vijana wa mpira wa wavu.
- 2019-08-24 11:50:53
Timu ya kitaifa ya vijana wa mpira wa wavu, chini ya miaka
19, inayoongozwa kiufundi na Hassan Alhussry imehakikisha ufuzu wake wa tatu
dhidi ya timu ya kitaifa ya Japan katika michuano ya dunia inayofanyika sasa
nchini Tunisia.
Timu ya kitaifa imehakikisha ushindi dhidi ya timu ya
kitaifa ya Japan kwa vipindi vitatu
vipindi viwili, wakati wa mechi za awamu ya tatu kutoka mashindano ya
kundi la tatu katika michuano ya dunia inayofanyika mnamo kipindi cha tarehe 21
hadi 30, mwezi huu wa Agosti.
Tija za vipindi zimekuja kama ifuatavyo : (25-19), (25-20),
(23-25), (25-15), (15-10).
Timu ya kitaifa inacheza katika kundi la tatu pamoja na timu
za kitaifa : "Ujerumani, Argentina, Mexico na Japan ".
Timu ya kitaifa imehakikisha ushindi katika awamu ya kwanza
dhidi ya timu ya kitaifa ya Ujerumani kwa vipindi vitatu dhidi ya vipindi
viwili, na hii ni kabla ya ufuzu katika awamu ya pili dhidi ya timu ya kitaifa
ya Argentina kwa vipindi vitatu kwa kipindi kimoja.
Orodha ya timu ya kitaifa ya Misri inajumuisha wachezaji
kama ifuatavyo : Abd Alrahman Alhusseny, Mohamed Elwan, Youssef Hussen, Mohamed
soliman, Ahmed Abd Alazeem, Ahmed Abas, Marwan Alnagar, Youssef Alantably, Anas
Mohamed, Ahmed Abdo, Mahmoud Osman, Karim Ibrahim, Iyad Mohamed, Omar Degham,
Ahmed Hanafy, Mohamed Oraby, Youssef Nosser, Youssef Gaafar na Ibrahim Raslan.
Ujumbe unaongozwa na Gaber Abd Alaty, huku timu hiyo
inaongozwa kiufundi na Hassan Alhussry na anasaidiwa na Nasser Ali kama kocha
msaidizi, na Mostafa Saleh kama mchambuzi wa kiufundi, na Nasser Hamdy kama
mkurugenzi Mtendaji, huku Dokta Mostafa Youssry anasimamia tiba ya mwili kwa
timu.
Comments