Wanaume na wanawake wa mpira wa kikapu 3×3 wanafikia robo ya fainali ya mashindano ya michezo ya Kiafrika.
- 2019-08-24 11:56:54
Timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa kikapu 3×3 kwa wanaume
na wanawake imefikia raundi ya pili katika mashindano ya michezo ya Kiafrika
yaliyofanyika sasa katika mji wa Morocco, Rabat.
Timu ya kitaifa ya wanaume, timu ya kwanza katika kundi lake
imefikia robo ya fainali leo, baada ya kushinda
mechi tatu dhidi ya timu ya kitaifa ya Madagascar kwa 22-18, kisha imeshinda timu ya kitaifa ya
Kenya kwa 21-16, pia imeshinda timu ya kitaifa ya Guinea ya ikweta kwa tija
21-7.
Timu ya kitaifa ya wanaume imeshinda jana dhidi ya timu ya
kitaifa ya Morocco kwa 19-15.
Huku timu ya kitaifa ya wanawake imefikia robo ya fainali
kama timu ya pili katika kundi lake baada ya kushindwa kwake leo toka timu ya
kitaifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa
18-15, lakini imeshinda jana timu ya kitaifa ya Guinea ya ikweta
kwa 17-4.
Timu ya kitaifa ya wanaume inajumuisha wachezaji kama :
Basem Alsaid, Karim Hisham, Mohamed Ibrahim na Mohamed TaHa chini ya uongozi wa
mkurugenzi wa ufundi Mohamed Samir.
Timu ya kitaifa ya wanawake inajumuisha wachezaji kama :
Farah Amr, Nada Gasser, Rana Abd Alzaher Na Maram Ahmed chini ya uongozi wa
mkurugenzi wa ufundi Haitham Safa.
Comments