Kwa ajili ya kutafuta njia za ushirikiano ... Waziri wa vijana na michezo anakutana na rais wa chama cha biashara na viwanda cha Ufaransa nchini Misri

 Dokta Ashraf Sobhy _waziri wa vijana na michezo _ amekutana na Mahmoud Alkassy rais chama cha biashara na viwanda cha Ufaransa nchini Misiri , hiyo kwa sababu ya kutafuta njia za ushirikiano baina wizara hiyo na chama katika programu kadha zinazowahudumia  vijana wa Misri .

 

Mkutano huo ulihudhuriwa na Manal Yousef _ mkuu wa idara kuu ya miradi na mafunzo ya vijana , Ahmed Afifi _ mkuu wa idara kuu ya miji ya vijana , Dalia Makled _ afisa wa masoko ya chama  cha biashara cha Ufaransa hapa Misri .

 

 

Mkutano ulijadili  ufafanuzi wa shughuli na programu za chama  hicho na mafanikio yanayofanywa kupitia kwa chama  ili kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kairo na Paris katika sekta mbalimbali za kiuchumi , wakati wa kukaribia kwa  Misri na Ufaransa .

 

Pamoja na ulijadili ufafanuzi wa ushirikiano kati ya  chama  hicho na taasisi ya kiufundi ya Ulaya , na kinachopewa na chama hicho kama programu na mikutano na haswa katika uwanja wa  mafunzo na ajira unaolenga kutoa fursa za kazi kwa vijana waliohitimu mafunzo .

 

Kwa upande wake , waziri wa vijana na michezo alikubali kushirikiana na chama cha biashara na uchumi cha Ufaransa nchini Misri, aliashiria kwamba inawezekana kushirikiana na chama cha biashara na viwanda cha Ufaransa nchini Misiri katika mafunzo ya vijana katika vituo vya vijana , na kufanyika mikutano ya kuajiri ndani majengo ya wizara , hiyo katika mfumo wa mkakati wa wizara ya vijana na michezo unaolenga kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana  na kuwaandalia soko la  kazi kusambamba na mpango wa Misri 2030.

Comments