Kituo cha Al-azhar cha
kupambana ugaidi kinauandaa mkutano kwa anwani "Nafasi ya Al-Azhar katika
kuimarisha Usalama na kupambana Ugaidi
barani Afrika" kwenye chumba kikubwa katika mji wa Buuth (wajumbe) wa
kiislamu jumanne 9/4.
Hiyo katika mpango wa
programu ya kusomesha na kuelewesha inayotolewa na Kituo kwa wanafunzi wageni
waafrika , jambo linalokwenda sambamba na uongozi wa Misri kwa Umoja wa
kiafrika .
Mkutano huu unahusu
umuhimu wa Kituo cha Al-Azhar wa kuziimarisha harakati za MIsri katika kutoa
misaada kwa bara la Afrika katika pande zote tofauti ; kimaendeleo, kiutamaduni
na kifikri, ili kuhakikisha mikakati ya maendeleo ya ajenda ya Umoja wa Afrika.
Comments