Wizara ya Vijana na Michezo yaanza matayarisho ya kukaribisha programu kubwa zaidi ya kujitolea Barani Afrika.

Wizara ya Vijana na Michezo itakaribisha na kuwahudumia kwa muda wa siku tano wajumbe wa AU ambao watawajibika kwa tathmini kama sehemu ya maandalizi yatakayofanywa kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika wa vijana wakujitolea, halmashauri “African Union Youth Volunteer Corps- (AUYVC)" mnamo Desemba 2019.

 

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukagua vifaa vya huduma ya vijana katika wizara na kujua uwezo na utayari wake. Halikadhalika pia kuangalia upeo wa uwezekano wa hafla hiyo kufanyika nchini Egypt.

Programu hiyo ya zoezi la vijana wa kujitolea ndiyo kubwa zaidi kwa mafunzo ya vijana wa Afrika ambamo Wanachama wa nchi za AU wanashindana.

 

Bwana Kokou Djagadou, mwanachama wa wajumbe wa AU wanaohusika na ukaguzi,walipongeza ukweli kuwa hafla hyo kwa mara ya pili chini ya miaka mitatu  itafanyika nchini Egypt, hvyo hatua hyo ni la kujizatiti na kupigiwa mfano vilevile kuangazia ukamilifu wa nchi hyo kujihusisha na kusaidia masuala ya vijana

Ziara ya ukaguzi ilijumuisha kuzuru kituo cha Vijana cha Al-Jazeera ambapo wajumbe wa AU walipokelewa na Ahmed Afif, sekreteri mdogo wa miji ya vijana wa wizara ya Vijana na Michezo,Meja Jenerali Ahmed Zakaria, Mkurugenzi wa kituo cha vijana cha Al-Jazeera,na Kamanda Sherif Mansour,Naibu wa Mkurugenzi wa kituo cha vijana cha Al-Jazeera.Wajumbe hao walihitimisha ziara ya ukaguzi katika kituo cha Olimpiki kama mojawapo ya vifaa muhimu vya kufanikisha hafla hiyo nchini Misri.

 

Wajumbe walionyesha kupendezwa na vifaa vya vijana vya Egypt na huduma zilizotolewa na nchi hiyo kwa njia  inayowasaidia vijana.Pia kiwango chake cha kuweza kujua na kutumia  shughuli zinazoeza kutolewa kwa wa Afrika,akipongeza jukumu la wizara ya Vijana na Michezo kwa kuinua kazi ya kujitolea kwa #Vijana katika Afrika, hivyo kujenga uwezo wa uongozi wa #Vijana wa #Afrika na kuwapa nafasi ya kupokea mafunzo kupitia #programu za kujitolea .


Comments