Kenya inaukaribisha mkutano wa kilele wa kiafrika ili kujadili Usalama wa chakula

 Kenya itakaribisha mkutano wa kilele wa kiafrika wiki ijayo ili kujadili mikakati mipya inayolenga kukuza usalama wa chakula   barani hilo wakati wa  kuwepo vitisho kwa afya ya binadamu .

 

Mwangi Keyongory , katibu wa baraza la mawaziri katika wizara ya kilimo , amesema kwamba serikali na mashirika ya kimataifa yameshirikiana katika mkutano wa Septemba 2-6  unaolenga kuongeza kujulikana kwa Usalama wa chakula huko Afrika . Kyongori alisema : maswala ya usalama wa chakula yako Mwanzoni mwa  nchi nyingi za Afrika , kenya inajivunia kushiriki katika mkutano wa kubadilisha mawazo na mazoea mazuri ili kuboresha vipimo vya chakula vinavyofaa barani .

 

Ameeleza kwamba wajumbe watajadili jukumu la mazoea na usalama wa chakula na kanuni za kupanga na vipimo katika kudhamini na kubana uwezo wa kushindana kwa bidhaa zinazopatikana kikanda" , aliongeza kwamba kenya imekusanywa nyuma ya juhudi za bara ili kuboresha miundombinu kwa usalama wa chakula kukiwa na ongezeko la biashara mipakani  katika bidhaa za kilimo kwa mfano kahawa,  chai,  nyama za ng'ombe,  sukari na samaki , aliendelea : " kenya inaendelea kuunga mkono kukuza vipimo vya usalama wa chakula barani Afrika wakati ambao bara linazingatia kuboresha afya ya mtumiaji " .

 

Kwa upande wake , " Peter Monya " , katibu wa baraza la mawaziri katika wizara ya biashara , amesema kwamba mkutano wa kilele ujao utazipa nchi za Afrika nafasi ya kujadili kuhusu siasa na maswala ya pesa ambayo ni muhimu kwa kukuza usalama wa chakula .

 

Monya ametaja kwamba kuna haja ya kuwekeza miundombinu ya kiwango cha juu kwa ajili ya kutathmini habari za kufuata kwa vipimo maalumu vya usalama wa chakula " , aliongeza kwamba uwekezaji katika miundombinu mpya kwa usafiri na kuhifadhi utakuza usalama wa bidhaa za kilimo zinazopatikana kwenye pande  za  kiafrika .

 

Inajulikana kwamba kenya inaukaribisha mkutano wa Afrika ili kujadili usalama wa chakula kwa mwanga wa biashara ya ndani kwa kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni ( WHO) na shirika la umoja wa matiafa  wa chakula na kilimo ( FAO ).

Comments