Waziri wa Vijana na Michezo anashuhudia Sherehe ya ufunguzi wa Oscar ya ubunifu wa kiafrika

 Waziri wa Vijana na Michezo Ashraf Sobhy alishuhudia sherehe ya ufunguzi wa Oscar ya ubunifu wa kiafrika, iliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika na matukio yake yataendelea hadi 10 Septemba, 2019 katika Kairo na Fayoum.

 

Na katika hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, alisema: "Sanaa ndio njia ya haraka zaidi ya kukaribiana kati ya watu na Chombo kizuri cha vyombo vya mawasiliano na daraja la kuongeza unganisho kati ya watu. Leo, tunasimama mbele ya vipaji vya vijana wa bara la kiafrika, ambalo tunakumbatia katika ardhi ya Kenanah Misri, kuwaambia ulimwengu wote kuwa bara letu la kiafrika limejaa nguvu za ujana ambazo zinahitaji kuwekeza na kuhamasisha zake. "

 

Waziri wa Vijana na Michezo: "Tumefurahi sana kuandaa tukio hili la vijana kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika, Wakati huo huo na Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika na katika mfumo wa Rais Abdel Fattah Sisi alitangaza Aswan kama mji mkuu wa vijana wa bara la kiafrika ."

 

Alisifu ushirikiano na Wizara ya Vijana na Michezo ya kimisri kutumikia vijana wa bara la kiafrika.Na mwakilishi wa Umoja wa Afrika alisifu wazo la Oscar, ambalo linakuja katika mfumo wa maono ya Umoja wa Afrika kuwekeza na kuhamasisha nguvu za vijana, akiashiria  kwamba bara la kiafrika siku hizi kuvutiwa na vijana kama msingi wa maendeleo.

 

Sherehe ya ufunguzi wa Oscar ya Ubunifu wa Kiafrika ni pamoja na idadi ya matoleo yiliyofanya na bendi ya Wizara ya Vijana na Michezo chini ya uongozi wa Dokta Maestro Hany Abdel Nasser, mbele ya wawakilishi wengine wa Umoja wa Afrika, na mabalozi wengi wa Kiafrika na wanahusika wa umma na wanaovutiwa na maswala ya Kiafrika na taasisi zinazofanya kazi katika maswala ya Kiafrika na wanachama wa Baraza la Wawakilishi, vyombo vya habari na waandishi wa habari.

 

Bendi ya Wizara ya Vijana na Michezo ilijumuisha  wimbo (You lost me) na Nagham Solyman, (Ta Fête Stromae )na Youssef Mohamed, (Turning tables) na Rodina Said, (la vie en rose/ alikuwa na nami) na Salma Omar ,Shorouk Muziki kwa Mwanamuziki Hany Mehanna, Mkusanyiko wa Muziki wa kiafrika tofauti (Top 20 saxophone songs | Sax House Music 2019، Wonderful Africa Chill out music، Sahalé – Magharib , The Spy From Cairo - Nafas, na wimbo mpya wa kikundi (Asili moja/ Of one origin) wa maneno ya mshairi Mahmoud Ismail, yaliyoundwa na Tamer Saad, Usambazaji na Ahmed Alaa, na kuimba Rodina Said, Nagham Suleiman na Salma Amr.

Comments