BENKI YA EXIM KULIPIA GHARAMA YA KUISHUHUDIA TIMU YA TAIFA STARS KATIKA AFCON 2019, MISRI
- 2019-04-11 00:42:53
Benki ya Exim leo imezindua kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.
Akizungumza wakati wa unzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Samaam leo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema kampeni hiyo ya miezi miwili itakamilika mwanzoni mwa mwezi Juni na ipo wazi kwa wateja wapya na wale ambao tayari wana akaunti za benki hiyo.
“Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki ya Exim katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.’’ Alisema.
Alisema washindi wa kampeni hiyo watapata fursa ya pekee ya kufurahia mchezo wanaoupenda huku pia wakipata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano hayo huku wakiwa wamelipiwa gharama zote za safari ikiwemo gharaza na Visa, tiketi ya ndege, gharamza za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu.
"Jumla kutakuwa na washindi watano ambapo washindi wawili watapatikana katika mwezi wa awali wa kampeni na washindi wa wengine watatu watapatikana katika mwezi wa mwisho wa kampeni hii.’’ Alisema
Comments