Siku 73 kuelekea fainali ya kuwania ubingwa wa taji la soka
baina ya mataifa ya Afrika nchini Misri, kamati andalizi inasema maandalizi
yanakwenda vizuri.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hany Abo Rida, ameiambia tovuti ya
Shirikisho la soka barani Afrika, cafonline.com kuwa, michuano hiyo itasalia
katika kumbukumbu ya mashabiki wengi wa soka wakati na baada ya kumalizika.
Misri itakuwa nchi ya kwanza, kuandaa fainali hii ambayo kwa
mara ya kwanza itakuwa na mataifa 24 katika michuano itakayofanyika kati ya
tarehe 21 hadi Julai mwaka 2019.
Tayari Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza kuwa
droo ya fainali hiyo itafanyika tarehe 12 mwezi Aprili.
Baadaye mwezi huu, michuano ya mwisho kufuzu katika fainali
hii, itachezwa katika viwanja mbalimbali.
Comments