Timu ya kitaifa ya wasichana wa Misri inashinda timu ya Puerto Rico mwanzoni mwa njia ya michuano ya dunia ya mpira wa wavu
- 2019-09-06 14:25:51
Timu ya kitaifa ya Misri ya wasichana wa mpira wa wavu imeshinda timu ya Puerto Rico kwa 3-1 mnamo siku ya kwanza ya mashindano ya kundi la kwanza katika michuano ya dunia inayoshikiliwa na Misri katika ukumbi wa shirikisho la mfereji wa Suez.
Tija za kipindi zimekuja kama ifuatavyo : (26-24), (25-20),
(30-28), (25-21).
Sherehe ya ufunguzi wa michuano imefanyika kabla ya mechi ya
ufunguzi moja kwa moja na kwa mahudhurio ya Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa
vijana na michezo na Hamdy Osman, gavana wa mkoa wa Ismailia na Osama Rabie,
mwenyekiti wa shirikisho la mfereji wa Suez na pia Amr Elwany, Mwenyekiti wa
umoja wa Afrika na naibu mwenyekiti wa umoja wa dunia wa michezo huu, na Ahmed
Abd Aldayem, mwenyekiti wa kamati inayoandaa michuano hiyo.
Kundi la kwanza la mashindano linajumuisha : Misri, Brazil,
China, Cameron na Puerto Rico.
Kundi la pili linajumuisha : Canada, Italia, Korea, Mexico
na Marekani.
Huku kundi la tatu linajumuisha : Argentina, Belarusi,
Romani, Urusi na Thailand.
Katika kundi la nne : Bulgaria, Congo, Japan, Peru na
Uturki.
Ukumbi wa shirikisho la mfereji wa Suez huko Ismailia
unashikilia mechi za kundi la kwanza na la pili, huku mechi za kundi la tatu na
la nne zitachezwa kwenye ukumbi wa 2 katika eneo la ukumbi zilizofunkiwa kwenye
uwanja wa Kairo.
Comments