Rais
Abdel Fattah al-Sisi ,siku ya Jumatano jioni 10,aprili,2019 alielekea mji mkuu
wa Jamhuri ya Cote d'Ivoire "Yamoussoukro" katika ziara ya kihistoria
ambayo ni ya kwanza kwa Rais wa Misri, baada ya kumaliza ziara yake kwa
Washington ,pembezoni mwa ziara yake ya nje iliyoanza siku ya Jumapili
iliyopita kwa nchi ya Guinea na itakayomaliza kwa ziara yake kwa Sengal.
Balozi
"Bassam Radi," Msemaji Rasmi kwa jina la urais amesema kuwa; Rais atafanya kikao cha mazumgumzo ya
kiwango cha juu pamoja na mwenzake Rais Alhasan Watara ili kujadili njia za
kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja zote na maendelea ya masuala ya
kikanda . Vilevile njia za ushirikiano za kuonyesha juhudi za Urais wa Misri wa
Umoja wa Afrika unaolenga kusukuma shughuli za maendeleo na mwingilio wa
kiuchumi barani .
Radi
alisisitiza kuwa ziara ya Rais huja katika mfumo wa azimio la Misri kuongeza
mawasiliano na ndugu zake wa kiafrika na kuendeleza kuimarisha uhusiano wake na
nchi za bara katika nyanja mbalimbali,hasa kupitia kuimarisha ushirikiano wa
pamoja katika nyanja za kiuchumi, kibiashara , kiuwekezaji pamoja na kipaumbele
cha juu kinachotolewa kwa masuala ya Afrika, hasa baada ya Urais wa Sasa wa
Misri wa Umoja wa Afrika.
Comments