Jiana Farouk alipewa medali ya dhahabu ya ligi la dunia la karate

 Jiana Farouk , mchezaji wa timu ya kitaifa ya kwanza kwa karate na bingwa wa klabu ya Ahli , alipewa medali ya dhahabu na nafasi ya kwanza katika michuano  ya ligi la dunia lililofanyika huko Japan , baada ushindi wake  mchezaji wa Ufaransa Lily Hertuo , katika mechi ya mwisho katika michuano ya uzito chini ya kilo 61 ,kwa 4_3 .

 

Ligi la dunia la karate  , ni  kituo kimoja  kinachotarajiwa kufikia  kikao cha michezo ya olimpiki kijacho katika Tokyo 2020. 

 

Jiana Farouk  jumamosi jioni alifikia mechi ya mwisho  baada ya  alimshinda mchezaji wa kwanza duniani , mchina Yin Yoan ( 5_0) katika nusu fainali. 

 

Jiana Farouk alikuwa amepata medali ya shaba katika mashindano ya kikao cha michezo ya kiafrika , yaliyofanyika karibuni huko Morocco .

Comments