kutambulisha utamaduni wa Rwanda katika Maktaba Kuu ya Kairo

Kituo cha kitaifa cha ukumbi wa michezo , muziki na sanaa ya kienyeji  (Folklore) , chini ya uongozi wa msanii “Yasser Sadek”, kwa kushirikiana na taasisi ya “El-Nile” ya masomo ya Kiafrika na Kimikakati, iliyoongozwa na “Mohamed Ezz El-din” , inaandaa mkutano wa tatu wa kila mwezi wa "Ujue familia yako", ili tujuane na tamaduni za Kiafrika ili  kusherehekea mwaka  wa (Misri - Afrika), katika maktaba Kuu ya Kairo, Zamalek, Saa moja  jioni Jumatano ijayo (11/9) .

   Mkutano huo utafanyika ili kujuana na utamaduni wa Rwanda kwa mahudhurio ya  balozi  wake “Saleh Habimana”, na idadi ya watu wanaohusiana na masuala  ya Kiafrika na watafiti wamisri.

   Mkutano huo utafanyika kwa mujibu ya juhudi kubwa zinazofanywa kwa Misri chini ya uongozi wa Rais “ Abd El-Fattah El-Sisi kwenye ngazi ya kiafrika , unaosambambana na juhudi za Serikali (nchi) za kueneza nafasi za  upendo na kuwasiliana na nchi za Kiafrika , na umefadhiliwa na Waziri wa utamaduni na chini ya usimamizi mkuu wa sekta ya mambo ya utoaji wa kitamaduni inayoongozwa na “Khalid Jalal” .

Comments