Misri inashinda medali 18 katika siku ya kwanza ya Mashindano ya kiafrika ya Kuogelea kwa wasichana
- 2019-09-13 14:37:31
Ujumbe wa kimisri unaoshiriki katika Mashindano ya kiafrika ya Kuogelea kwa vijana ulishinda medali 18 katika mwisho wa siku ya kwanza ya mashindano uliyongozwa kwa Tunisia, na utaendelea hadi Septemba 15.
Mhandisi Tarek Bakry, naibu wa Shirikisho la Kuogelea la kimisri na mkuu wa timu ya Misri, alisema katika taarifa ya waandishi wa habari kwamba timu hiyo ilifanikiwa kushinda medali 4 za dhahabu, 9 za fedha na 5 za shaba wakati wa siku ya kwanza ya mashindano, akaongeza kuwa karibu na waogeleaji 23 watafikia kushiriki katika siku ya pili ya mashindano ambapo waogeleaji 350 kutoka nchi 35 za Kiafrika wanashindana.
Bakry aliisifu maandalizi kwa mashindano hayo, akisisitiza kwamba upande wa Tunisia unashirikiana kwa kiwango cha juu na unafanya kazi kutoa njia zote za starehe kwa ujumbe unaohusika katika mashindano hayo.
Ni muhimu kukumbuka kuwa toleo la kumi na tatu la Mashindano ya Kuogelea ya Kiafrika ya vijana ilianza asubuhi hii nchini Tunisia, na inatarajiwa kuona ushindani mkali na kuwepo kwa nchi zinazoongoza katika mchezo huu, kama vile Misri, Afrika Kusini, Algeria, Morocco na Zimbabwe.
Comments