Kwa ajili ya mataifa ya kiafrika..…. Lango la Misri la vijana na michezo ... kwa lugha nne
- 2019-04-15 13:39:12
Waziri wa vijana na michezo,DKT. Ashraf Sobhy
amekubali kuanzisha lango la kielektroniki lililopo chini ya wizara ( lango la
Misri la vijana na michezo ) kwa lugha nne nazo ni (lugha za kiarabu,
kiingereza, kifaransa, na Kiswahili) .
Hiyo ni kutayarisha kwa ajili ya
mashindano ya kombe la mataifa ya kiafrika ambayo yatafanyika nchini Misri
mnamo katikati ya mwezi wa Juni ujao kwa
ajili ya kuwasiliana na vijana wa Misri na wa Afrika ndani na nje.
Mwanahabari, BW. Gamal Nur EL-din, mkuu wa
gazeti la lango amesisitiza kuwa uamuzi wa waziri wa michezo wa misri unakuja katika wigo wa mkusanyiko wa
huduma mbali mbali zinazotolewa na
wizara hiyo kwa ajili ya kuyafanikisha mashindano ya kiafrika. Ambapo lango hili litaanzisha kwa lugha hizi
nne kwa ajili ya kuwasiliana na vijana
wa nchi 24 za kiafrika zinazoshiriki katika mashindano haya. Na ameongeza kuwa lango hilo la kielektroniki
halitaishia katika kutoa huduma za michezo na kutangazia michuano na mazungumzo
ya wachezaji wa mpira pamoja na habari zao,
bali linaelekea pia katika kuyatambua maeneo na namna ya kuhudhuria mechi na
kutoa matembeleo ya kiutalii na ya mabaki ya kale ya kila mkoa katika mikoa
yote itakayokaribisha makundi 6 ya mashindano hayo, pia umekuisha kuanzisha
ukurasa maalumu wa mashindano.
Aidhaa kutatimia kuanzisha idhaa ya
kielektroniki kwa jina la vijana wa misri. Idhaa hii itajumuisha sehemu kubwa
kwa ajili ya kutangazia mashindano. Pia kumetimia kutoa mafunzo kwa ajili ya
wasichana na wavulana 25 kutoka vitivo
vya habari na wahitimu wake na wenye vipaji kutoka vitivo vingine ili wawe
chimbuko la watangazaji wa siku za usoni
na ongezeko jipya linatolewa na wizara
ya vijana kwa habari ya kimisri.
Mhariri mkuu wa gazeti la Bawaba amesisitiza kwa kusema kwamba baada ya utulivu
wa kiusalama nchini Misri hivi karibuni na kurudi kwake kuliongoza bara la
Afrika pamoja na kuwasiliana na vijana,
waziri wa michezo ametangaza kwamba lango hilo linazingatiwa kuwa ni njia ya habari inayokusanya zaidi kwa ajili ya
kuwasiliana na vijana kwa kuzingatia kuwa ni nyumba na njia yao . Na hayo kupitia huduma zinazotolewa na
wizara hiyo. Pia litakuwa ni daraja la mawasiliano pamoja na vijana wetu nje sawa
ya wageni miongoni mwao na wahamiaji ili kuijua Misri kwa ukaribu katika maswala yote na pahala pa kiutalii na
huduma na mashindano ambayo Misri inaishriki pamoja na historia ya mashujaa wa
misri kwa kifupi katika vyombo vyote vya habari.
VileVile waziri wa vijana na michezo, DKT.
Ashraf Sobhy amesisitiza kwamba lango la kielektroniki linazingatiwa kuwa ni
mfumo kamili wa habari unawahudumia vijana wa misri ndani na nje. Na litakuwa ni daraja la mawasiliano baina ya
vijana wa misri na wa Afrika.
Waziri wa michezo wa misri ameongeza kuwa
wizara itafanya kazi juu ya kutoa huduma
mpya kwa ajili ya mashindano ya kombe la mataifa ya kiafrika yatakayofanyika
nchini Misri na zitaanza kwa lugha hizi nne ili kujenga picha ya yanayotokea
katika uwanja za mashindano hayo, na kutoa huduma kwa mashabiki wa kiafrika
watakaohudhuria mechi. Na kuzungumza na mataifa yote ya kiafrika kwa lugha zao.
Ambapo njia ya karibu zaidi katika kuwasiliana na mwengine ni kuzungumza naye kwa lugha yake si kwa
lugha yetu ya kiarabu.
VileVile ameongeza kuwa Misri inafanya kazi juu
ya kuyafanikisha mashindano hayo kwa pande zake zote. Na kwamba vyombo vya
habari vinazingatiwa kuwa ni njia ya
karibu zaidi katika kujenga picha ya mafanikio yanayotokea katika hali halisi. Kwa hivyo
tutatoa huduma mbali mbali kwa vijana wa
Afrika kabla ya mashindano, wakati wa
mashindano na baada ya mashindano. Licha ya huduma zinazotolewa na taifa nafasi ya Misri barani Afrika.
Comments