Kampeni ya matangazo kwa ajili ya mafanikio ya kimisri kupitia shughuli za wiki ya kibiashara huko Tanzania
- 2019-09-15 11:58:55
Taasisi ya maendeleo ya bidhaa za nje ilipanga kampeni ya matangazo kwa wiki ya kibiashara ya kimisri huko Tanzania kwa kuweka mabodi kuhusu mafanikio ya Misri na hivyo kwenye njia mashuhuri zaidi katika mji mkuu wa Tanzania na kwenye magazeti muhimu zaidi ya kitanzania kwa lengo la kuvutia watalii na makampuni ya kitanzania na kiafrika , taasisi kutoka kwa kampeni ya matangazo ililenga kujua makampuni ya kimisri kupitia shughuli za wiki ya kibiashara ya kimisri huko Tanzania kama mpango wa taasisi ili kutangaza wiki za kibiashara barani Afrika .
Wiki ya kibiashara ya kimisri ya kwanza ilifanyika huko
Tanzania katika kipindi cha 10 hadi 14 septemba kwa ushirikiano wa makampuni
kumi na nne ya kimisri , ilifunguliwa na waziri wa biashara ya Tanzania na
Mohemed Gaber Abo El Wafa balozi wa Misri huko Tanzania na Mohemed Abdel Megiid
mkuu wa ofisi ya kibiashara ya kimisri huko Tanzania , na Ahmed Abdelgawad
mwakilishi wa taasisi ya maendeleo ya bidhaa za nje na maneja wa wiki
kibiashara pamoja na maafisa wengine katika nchi ya Tanzania .
Maandalizi ya taasisi kwa tukio hilo yalikuwa katika mfumo
wa juhudi za wizara ya biashara na viwanda ili kuinuka uwezo wa kuuza bidhaa
kwa makampuni ya kimisri kupitia kupata nafasi nzuri za bidhaa za kimisri ili
kusambaza katika masoko ya kiafrika na haswa wakati wa utawala wa Misri kwa
shirikisho la kiafrika mwaka huo.
Soko la Tanzania ndilo ni mojawapo ya masoko muhimu sana kwa
bidhaa za kimisri , haswa kwamba Tanzania ni memba muhimu baina nchi za Afrika
mashariki na SADC na inazingatiwa mhimili muhimu kwa masoko ya nchi za Afrika
mashariki na kusini .
Ni muhimu kutaja kwamba bidhaa za nje za kimisri kwa
Tanzania zilihakikisha mwaka uliopita ongezeko kubwa kwa asilimia 21 , ambapo
thamani yake ilikuwa dola milioni 35.5 , kulingana na mwaka 2017 ilikuwa dola
milioni 29.1 , mizani ya biashara inaelekea baina nchi hizo mbili kwa maslahi
ya misri kwa thamani ya dola milioni 30.9 , jambo linalosisitiza uwepo wa fursa
kubwa ili kupenya bidhaa na usafirishaji wa kimisri kwa masoko ya kitanzania
haswa katika nyanja za mbolea , kemikali , viwanda vya chakula , vifaa vya afya
, kauri , saruji na viwanda vya umeme.
Comments