Itifaki ya ushirikiano kati ya wizara ya vijana na michezo, Muugano wa mpira na baraza la utamaduni wa Uingereza ili kufundisha ustadi wa mpira wa miguu ya wanawake

Wizara ya vijana na michezo imewakilishwa kwa idara kuu ya maendeleo ya kimichezo imefanya mkutano pamoja na Dokta Sahar Abd Alkalek, Mwanachama wa baraza la uongozi wa Muungano wa Kimisri wa mpira wa miguu na wawakilishi wa baraza la utamaduni wa Uingereza nchini Misri, ili uteuzi wa timu ya taifa kwa kila mkoa katika mpira wa miguu ya wanawake na kufanya kikao cha kuifundisha ustadi wa mpira wa miguu mwishoni mwa mwezi wa Oktoba ijayo, hii katika mfumo wa mradi wa wasichana 1000  ndoto 1000, ili kushiriki katika ligi na mashindano yote mengine.

Hii inakuja katika mfumo wa ushirikiano na ushiriki kati ya wizara ya vijana na michezo ya Kimisri, baraza la utamaduni wa Uingereza na muugano wa Kimisri ya mpira wa miguu ya wanawake, imetajwa kuwa mradi huo umetekeleza tangu mwaka iliyopita katika mikoa ya juu ya Misri kuanzia mkoa wa Beni Suef na kupita kwa mikoa ya Menya, Assiut, Sohag, Qena na Luxor hadi Aswan na Alwadi Aljadid kwa jumla ya wanawake 1000, pia wakufunzi waliopata kikao cha (primer skills) wliowafundishwa hapo awali kwa wizara ya vijana na michezo na baraza la utamaduni wa Uingereza, kutoka wizara ya vijana na michezo wamehudhuria Dokta Sonya Donia, mkurugenzi mkuu wa msingi wa watu na Ahmed Shabaan, mratibu mkuu wa mradi.

Na kutoka baraza la utamaduni wa Uingereza wamehudhuria Youssr Goda, mkurugenzi wa mipango ya baraza na Nancy Alamir, mkurugenzi wa mradi.

Comments