Michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika 2019 AFCON itafanyika nchini Misri, kuanzia Juni 15 hadi
Julai 13, bodi ya uongozi ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) imeamua leo
Jumanne Januari 8 mjini Dakar.
CAF imeamua kuteuwa Misri badala ya Afrika
Kusini. Awali Cameroon ilitarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hii ya AFCON 2019,
ambayo itajumuisha timu kwa mara ya kwanza timu 24 badala ya 16.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
itapigwa kwa mara ya tano katika historia yake katika ardhi ya Misri, baada ya
mwaka 1959, 1974, 1986 na 2006. Uamuzi huu umechukuliwa na bodi ya uongozi ya
Shirikisho la Soka la Afrika (ComEX), iliyokutana tarehe 8 Januari 2019 katika
mji mkuu wa Senegal, Dakar.
ComEx imeteua Misri kama mwenyeji wa
michuano ya AFCON 2019 badala ya Afrika Kusini, nchi nyingine iliwania kuchukua
nafasi ya Cameroon.
Hata hivyo hali ya usalama nchini Misri
bado suala linaloendelea kujadiliwa na viongozi wa CAF. Lakini
viongozi wa Misri wamesema suala hilo litapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Comments