Eneo la kijiografia
Mji wa Ismailia unazingatiwa kuwa ni miongoni mwa
miji ya mfereji. Nao ni mji mkuu wa mkoa wa Ismailia. Idadi ya wakaazi wa miji
na mitaa yake inakadiriwa kwa watu milioni. Mji huu umejengwa kwenye ukanda wa magharibi
wa ziwa la mamba ambao unazingatiwa kuwa ni
moja ya sehemu za mhimili wa mfereji wa Suweiz ili uwe kituo cha mamlaka
ya mfereji wa Suweiz mnamo zama ya sultani Ismail.
Baada ya ongezeko la
wakaazi katika nyakati za hivi karibuni, mji ule umeyashuhudia mabadiliko
kadhaa miongoni mwayo; kuanzisha barabara ya chini ya ardhi ya Jamal Abdi
EL-Naasir katika kituo cha mji , ukiongezea na "MJI WA EL-MUSTAKBAL"
ili kukidhi ongezeko la wakaazi na mji
huu upo barabara ya kairo ya Ismailia jangwani. VileVile mkoa huo ulianza
kufanya upya na kujenga madaraja mapya juu ya mfereji wa Ismailia. Aidhaa mkoa
huo unapambanuka kwa bustani nyingi na
matembeleo ya kimaumbile.
Historia kwa ufupi
Uanzishaji wa mji huo unarejea katika zama za kabla ya
familia. Mitume, Ibrahim, Yussf, Yakobo na Musa
walipita katika ardhi yake. Ulipata heshima kubwa ya kutembelewa na familia takatifu. Uislamu
uliingia humo ukiambatana na ufunguzi wa
kiarabu chini ya uongozi wa Amru bin Aasiy. Ulianzishwa rasmi katika zama
ya Said Pasha tarehe 27 Aprili 1862. Kila mwaka, unasherehekea sikukuu yake ya
kitaifa tarehe 25 Januari kuendeleza kumbukumbu ya ari ya majeshi yake dhidi ya
majeshi ya kiingereza mwaka 1952.
Matembeleo ya
kimaumbile na ya kiutalii
Mji huo unatoka katika
kingo mbili za mfereji wa Suweiz na maziwa yenye maji chumvi Pamoja na ziwa la mamba. Kwa kuangalia hali yake ya hewa ya wastani
kwa muda wa mwaka mzima , licha ya kuwa ni karibu na mikoa ya kairo,
Kaliyubiyah na Sharkiyah unayatumia
maeneo ya mapumziko ya majira ya joto na ya baridi.
VileVile una makusudio
mengi ya kiutalii ya kihistoria yanatuhisisha utukufu wa ustaarabu wa kimisri
pamoja na yanatukumbusha shindi zilizo
tukuka. VileVile alama zake za kihistoria
zinazoonekana kama mchoro mzuri wa uzuri unaotoa fursa kwa watalii
kuyaishi pamoja na safari ya kihistoria katika ardhi yake. Na miongoni mwa
matembeleo haya ni :-
Makaburi ya
Commonwealth
Makaburi haya
yanaenea sana katika maeneo mbali mbali nchini Misri. VileVile yanawavutia watalii wengi wanaokuja ili kutembelea jamaa zao.
Kumbusho la mabaki ya kale
Linazingatiwa kuwa
ni miongoni mwa makumbusho ya kale zaidi yaliyojengwa na wahandisi
waliofanya kazi katika mamlaka ya
mfereji wa Suweiz mwaka 1911.
Kumbusho la DELSEBS
Uanzishaji wake unarejea katika kipindi cha uchimbaji wa
mfereji wa Suweiz mwaka 1859. Lilikuwa
makazi ya kuishi mhandisi wa kifaransa
Ferdinad Delesebs. VileVile linajumuisha
vyombo vyake na viambata vyake vya michoro ya kiuhandisi.
Kumbusho la polisi
Linapatikana usimamizi
wa usalama wa Ismailia. Linajumuisha silaha mbali mbali zilizotumiwa na
majeshi ya kimisri ili kupiga vita
majeshi ya kiingereza katika mwezi wa Januari 1952.
Mlima wa KAFRYA na
AI-SAIDI
Upo kijijini
Abu Khalifa. Na kijiji hiki kinazingatiwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ya
kizamani muhimu sana yanayorejea katika zama ya kiyunani na ya kirumi.
Mlima wa EL-SAHABA na
EL-AZBA
Upo kusini mwa Abu
Suir umbali wa takribani kilomita mbili. Unajumuisha mabaki ya kale yanarejea
katika zama ya kiyunani na ya kirumi.
Mlima wa ABU SAIFI
Unapatikana umbali
wa takribani kilomita tano kutoka mashariki mwa Qantara. Unajumuisha
vipande vitatu vya mabaki ya kale vinarejea katika zama ya kiyunani na ya
kirumi.
Mlima wa EL-HABR
Upo umbali wa
takribani kilomita 75 kutoka mashariki mwa Qantara. Unajumuisha ngome tatu za
kizamani zinarejea katika zama za mwisho za kifarao na wabatalima na
waromani.
Comments