Timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa wavu iko kwenye kambi iliyofungwa ya maandalizi ya michuano ya dunia nchini Japan

 Ujumbe wa timu ya kitaifa ya kwanza ya mpira wa wavu, chini ya uongozi wa mkurugenzi wake wa kiufundi (Gedo Foromolen) umeelekea mji wa Hiroshima nchini Japan, ili kuingia katika kambi iliyofungwa ya maandalizi ya michuano ya kombe la dunia.

 

Orodha ya timu yetu ya kitaifa inajumuisha : Abdallah Abd Alsalam, Hosam Youssef, Ahmed Salah, Hisham Youssry, Mohamed Adel, Rashad Shebl, Abd Alrahman Soudy, Mohamed Abd Almosen, Ahmed Said, Omar Naguib, Ahmed Diaa, Mahmoud Mansour, Ahmed Abd Alaal na Mohamed Reda.

 

Michuano itafanyika mnamo kipindi cha tarehe 1 hadi 15, mwezi wa Oktoba ijayo nchini Japan.

chombo cha kiufundi cha Mafarao kinajumuisha : Gedo Foromolen kama mkurugenzi wa ufundi, Ahmed Ashour kama kocha mkuu, Daktari Sameh Dhlaam kwa tiba ya mwili, Ragab Kotb kama mchambuzi na Sharif Alshmrly kama meneja wa timu.

Comments