Kituo cha Olimpiki kinakaribisha Mashindano ya kiarabu ya Ndondi mwezi ujao wa Februari

 Kituo cha Olimpiki huko Maadi kitakaribisha Mashindano  ya  kiarabu kwa Ndondi kwa vijana , wazaliwa mnamo 2002-2003, yaliyopangwa kufanyika mwezi ujao wa Februari nchini Misri.

 

Mohamed Abdel Aziz Ghonaim, mkurugenzi wa Shirikisho la Ndondi, alithibitisha kwamba mashindano hayo yatafanyika katika Kituo cha Olimpiki, ambacho kilishiriki toleo la mwisho mwaka jana na kufanikiwa sana na ushiriki wa idadi kubwa ya nchi za Kiarabu.

Mkutano mkuu umepangwa kufanywa Septemba 28 kujadili bajeti na maandalizi ya mwisho.

 

Mkutano Mkuu pia unashuhudia kupitishwa mpango mpya wa msimu mpya, unaopangwa kuanza Oktoba ijayo kwenye Mashindano ya Jamuhuri kwa watu wazima, ambao ni michuano ya kwanza ya msimu mpya kwa msimu wa ndani "kienyeji " 2019/2020 mnamo kipindi cha tarehe 5 hadi 10 Oktoba huko Assiut.

 

Imepangwa kufanyika Mashindano ya Jamhuri kwa vijana  kutoka 2 hadi 7 Novemba huko Aleskandaria na ushiriki wa idadi kubwa ya wachezaji.

Comments