Waziri wa michezo anawaomba wachezaji wa kuinua uzito wazingatie katika mazoezi ... Wizara na olimpiki hutatua tatizo hili

 Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alikutana na kikundi cha mabingwa wa Misri wa kuinua uzito na wafanyikazi wa kiufundi , ili kueleza jukumu la nchi ya Misri huwakilishwa na wizara ya vijana na michezo kwa ushirikiano na kamati ya olimpiki katika utatuzi wa tatizo la kusimamisha shirikisho la kimisri la kuinua uzito duniani , na kuwahimiza kuendelea mipango yao ya mafunzo .

Mkutano ulihudhuriwa na kocha Mohamed Mosa Meneja wa kiufundi kaa timu ya kuinua uzito , kocha Tharwat Bendary Meneja wa kiidara kwa timu hiyo na kocha Mohamed Hosny kapteni mkuu , na wachezaji " Mohemed Ehab , Mohemed Selim , Ahmed Ashor , Sara Samir , Halima Abdelazim n'a Samar Habashy "

Waziri wa vijana na michezo alieleza kwamba hatua kadhaa za kirasmi zilizochukuliwa kwa kushirikiana na kamati ya  olimpiki ya kimisri , na kutafuta njia mbalimbali ili kutatua tatizo la kusimamisha shirikisho la kimisri la kuinua uzito ulimwenguni .

 

Waziri aliwaomba mabingwa wa Misri wazingatie hata kukamilisha makambi yao ya mafunzo kulingana na mipango yanayowekwa kwao   ili wajiandae ubingwa ujao hadi tatizo hilo liishe , akiashiria umuhimu wa kuhifadhi kiwango cha kiufundi kwa wachezaji kupitia kufanya mazoezi binafsi kwa kila mchezaji katika mfumo wa kustahili na kujiandaa kwa mashindano tofauti .

Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba atoe msaada wote kwa mabingwa wa Misri wa kuinua uzito wanaohakikisha mafanikio mazuri katika sherehe za kimataifa , akielezea  matumaini yake kuwa  Mwenyezi Mungu atasaida wizara na kamati hiyo kutatua tatizo la kusimamisha shirikisho la  kuinua uzito la kimisri , na kuanza kushiriki mabingwa wa Misri katika michuano ya kimataifa  inayofikia kikao cha michezo ya olimpiki huko Tokyo 2020 .

Comments