Hilmi Shaarawy: «Mwaminifu wa tamaduni za Kiafrika »

Tangu alihitimu masomo yake ya shemu ya jamii katika Chuo Kikuu cha kairo mwaka wa 1958, na anaitilia manane Afrika kwa sababu ni upana  wa kijiografia na kitaifa kwa Misri, akifahamu umuhimu wa kutosahau ndugu zetu wa Afrika katika hali za  kisiasa kwa sababu ya mahali na wakati na masuala ya pamoja . yeye ni Mohamed Hilmi Shaarawi, mwana wa kisiasa , wa kushoto na mmisri , Mjuzi  wa Mambo ya Afrika , na  Mwanzilishi wa Kituo cha tafiti za Kiarabu na Kiafrika.

Yeye ana michango kadhaa kuhusu mambo ya Afrika, miongoni mwake; alikuw  mkuu wa harakati za uhuru wa Afrika huko Misri mwaka 1975 , profesa wa sayansi za kisiasa katika Chuo Kikuu cha Juba huko Sudan (1981-1982), mtaalamu wa mahusiano ya Kiarabu na kiafrika katika Shirikisho la Uarabu la Elimu na Utamaduni na Sayansi huko  Tunisia  (1982-1986). , Na Rais wa zamani wa jumuia ya Afrika ya Sayansi za kisiasa.

Lakini sasa, yeye ni Katibu wa Kamati ya Ulinzi wa Utamaduni wa Taifa nchini Misri na Mkurugenzi wa Kituo cha tafiti za Kiarabu na kiafrika.

 

Pia ana makala na chunguzi kadhaa  juu ya Afrika, hususan: "Obama, hotuba yake ya Kiafrika, ajenda ya Afrika ya kilele cha  Kiarabu, Chad kama Waarabu, Somalia pia ni wajibu wa Kiarabu," na maono ya kimkakati ya mahusiano ya Kiarabu na Afrika,na  mgogoro wa maji ya Nile. Utandawazi wa miradi ya maji, na kuhujiana na harakati za Uislamu wa kisiasa.

Kutia manane kwake kuhusu mambo ya Afrika kulimfanya mmoja wa wataalam maarufu zaidi, lililosababisha  kuwa Wizara ya Utamaduni inayoongozwa na mwandishi wa habari na Waziri wa Utamaduni Hilmi Al-Nunem, iliifanya sherehe maalum ili kushukuru juhudi zake za kiutafiti chini ya kichwa "Hilmi Shaarawi .. safari ya kutoa(atia) ", iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Utamaduni kwa ajili ya kumheshimu juu ya juhudi zake na kuimarisha kwake kwa tamaduni za Kiafrika kwa ujumla na utamaduni wa Misri hasa, ambapo idadi kubwa ya watafiti na wataalam katika mambo ya kitamaduni kutoka Misri na nchi kadhaa za Kiafrika na Kiarabu walishiriki, Januari  ,2018.

Pia aliheshimiwa na Dkt  Ashraf  Sobhi huko "shule ya kiafrika  2063" Desemba ,2018.

Vitabu vyake muhimu Zaidi :

Kitabu cha Utamaduni na wasomi katika Afrika.

Helmi Shaarawy:  Kitabu cha wasifu ya kimisri na kiafrika.

Comments