Waziri wa vijana na michezo anakutana na ujumbe wa viongozi wa vijana wa Saudi hapa Misri

 Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alikutana leo na ujumbe wa viongozi wa vijana wa Saudi Arabia uliopo nchini Misri katika mfumo wa programu ya mabadiliko ya viongozi wa vijana  baina ya Misri na ufalme wa kiarabu wa Saudi.

 

Sobhy alipokea ziara ya ujumbe wa kiarabu wa Saudi katika Misri na kiongozi wao Bwana Mohemed Bin Ahmed Bin Othmane mkuu wa ujumbe huo , akiashiria kina wa mahusiano baina ya Misri na Saudi Arabia , pia akisisitiza umuhimu wa kupata faida ya maoni ya waheshimiwa wabunge wa ujumbe wa Saudi Arabia kwa lengo la kuendeleza mpango huo na kuuboresha , ili kuongeza uzoefu wa nchi mbili na ujuzi wa kudumu baina ya vijana wa Misri na wa Saudi Arabia.

 

Inapaswa kutajwa kwamba ujumbe huo unapokelewa kwa Misri katika kipindi cha 21 hadi 30 Septemba 2018 , wakati huohuo ujumbe utafanya mikutano mengi na ziara mbalimbali mkoani Kairo na Sharm El sheikh .

Comments