Wizara ya vijana na michezo inaendelea shughuli za jukwaa la vijana wa Kiafrika kwa bonde la Nile chini ya kauli mbiu (Nile moja, Taifa moja)
- 2019-09-25 13:16:59
Wizara ya vijana na michezo inaendelea shughuli za jukwaa la vijana wa Kiafrika kwa nchi za bonde la Nile chini ya kauli mbiu (Nile moja, Taifa moja) mnamo kipindi cha tarehe 21 hadi 27, mwezi wa Septemba katika miji miwili ya Luxor na Aswan kwa ushiriki wa nchi 11 za Kiafrika ( Misri, Ethiopia, Sudan, Uganda, Burundi, Kenya, Congo, Rwanda, Eritrea, Tanzania na Sudan Kusini).
Jukwaa linalenga kwa umoja wa mawazo ya vijana
wa Kiafrika na kutoa mawazo ya vijana ili kutatua matatizo mengi na shida za
nchi za Kiafrika na kutambua kwa vyanzo vya vitisho vinavyokabili mataifa ya
Kiafrika na kubadilishana mawazo kati ya vijana wa Kimisri na wa Kiafrika.
Wizara ya vijana na michezo imetekeleza
programu ya kitalii ya wajumbe wanaoshiriki kwa mkoa wa Luxor na kutembelea kwa
hekalu la mfalme Hatshepsut, hekalu la Habo na hekalu la Luxor.
Comments