Kwa siku ya pili, programu ya mafunzo kwa Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar inajadili tabia na sifa za mhusika mwenye msimamo mkali

Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar kwa kupambana Msimamo mkali kiliendelea na programu yake ya mafunzo ya kwanza  kwa  wanafunzi  na wahitimu  wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar mnamo kipindi cha Septemba 29 hadi 3 Oktoba chini ya kichwa cha : "Uwiano wa uzushi wa Msimamo mkali na hatari zake".

 

 Mnamo siku yake ya pili kupitia hotuba ya Dokta .  Walid Bilal, na Dokta  Mohamed Abdel Rahman, watafiti katika Kituo cha uangalizi cha Al_Azhar ,  programu ilijadili tabia na sifa za  mhusika mwenye msimamo mkali huko Ulaya na Afrika, na vile vile sababu na nia za msimamo mkali na ugaidi.

  Kama Dokta  Rajab al-Naghi, mtafiti katika  kituo cha Al-Azhar , alijadili jukumu kubwa  la Al-Azhar katika kueneza utamaduni wa Usamehe , Amani na kupambana na msimamo mkali wa ndani na nje naye alionyesha njia za kisayansi maarufu zaidi ambazo kupitia kwake jamii inaweza kulinda vijana toka kujihusisha katika mawazo yenye msimamo mkali..

Comments