Doaa Al-ghobashy, bingwa wa mpira wa wavu anaonekana katika mada ya Kiingereza ya awamu ya kwanza katika shule ya kimsingi

 Doaa Al-ghobashy, bingwa wa timu ya kitaifa ya mpira wa wavu wa Pwani na anayeshinda medali ya kidhahabu ya kikao cha michezo ya Kiafrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Morocco ameonekana katika mitaala ya elimu.

 

Wizara ya elimu imeweka aya juu ya Doaa Al-ghobashy katika kitabu cha Kiingereza cha shule ya kimsingi  na juu ya sifa zake za urefu na kiwango cha mchezo, na aya hii ni : " mchezaji wangu mpendwa , bingwa Doaa Alghobashy, mchezaji wa timu ya kitaifa ya mpira wa wavu, yeye ni mrefu sana, ambapo urefu wake ni centimeter 180,  mwenye nguvu, mwepesi, anaweza kuruka juu, mzuri, ana tabasamu kubwa."

 

Kwa upande wake, Doaa Al-ghobashy, bingwa wa timu ya kitaifa ya mpira wa wavu wa Pwani ameelezea furaha yake baada ya kuonekana kwake katika mitaala ya elimu, akisisitiza kuwa hatua hiyo imempa kichocheo ili kukuza kiwango chake na kuzidisha juhudi zake ili kushinda michuano zaidi.

Comments