chuo kikuu cha Alaeskandaria kinatoa udhamini 17 kwa wanafunzi wa Burundi mnamo 2019

Mkurugenzi wa chuo kikuu cha ALESKANDARIA Dokta  Essam El kurdi alitangaza kuwa wanafunzi 17 kutoka Burundi watapewa udhamini wa masomo ya Uzamili na Uzamivu  kwa mwaka wa masomo 2019 /2020 katika chuo kikuu cha Aleskandaria ( wanafunzi 14 katika kitivo cha Tiba na wanafunzi 3 katika kitivo cha Biashara) hii inakuja kama sehemu ya udhamini ya nchi za bonde la nile kutoka chuo kikuu cha Aleskandaria mwaka huu kwa masomo yaUzamili na Uzamivu  unaofikia udhamini 133.

kwa mujibu wa taarifa jumanne 1/10 mkurugenzi wa chuo kikuu alipokea barua ya shukrani kutoka kwa balozi wa Misri" Abeer Bassiouni Radwan " kwenda Burundi kwa udhamini unaotolewa na chuo kikuu cha Aleskandaria kwa wanafunzi wa Burundi

katika mkutadha huo huo "El kurdi" aliwakaribisha wanafunzi kutoka Burundi kusoma katika chuo kikuu cha Aleskandaria alisisitiza hamu ya chuo kikuu katika kuwezesha taratibu zote kuvutia wanafunzi wa kimataifa hasa wanafunzi wa bara la Afrika baada ya urais wa Misri wa umoja wa kiafrika .

alieleza kuwa chuo kikuu kinachukua mkakati katika kuenea elimu ya juu kwa kufungua kukubali wanafunzi kutoka nje ya Misri na kuwahimiza wasome katika vitivo tofauti vya chuo kikuu.

pia huwapatia msada kamili kwa njia ya ofisi za wahamiaji katika vyuo vyote kama mabalozi wa Misri nje ya nchi , aliongeza kuwa chuo kikuu kinajitahidi kila wakati ili kuendeleza kanuni za masomo kulingana na hali ya hivi karibuni ya mtindo ya kisayansi na kitaaluma

kwa upande wake , balozi  huyo alialika wanafunzi wa  Burundi wanaotaka kusoma nchini Misri kuwasiliana moja kwa moja na vyuo vikuu vya Misri kupitia mtandaoni

alipendekeza pia kutiwa saini kwa makubaliano ya mapatano kati ya chuo kikuu cha alexandria na chuo kikuu cha bujumbura (chuo kikuu cha umma tu nchini burundi ) na tushirikiane nao kufungua kitivo cha Dawa na kitivo cha Tiba ya mifugo kwa sababu ya hitaji  la kada kufungua tena

Comments