Wizara ya michezo ya Misri
pamoja na shirikisho la soka nchini humo wametangaza kuwa tayari kwa mashindano
ya kombe la mataifa ya Afrika yanayoanza Juni 15.
Achraf Sobhi ni Waziri wa michezo.
"kutakuwa na kamati kuu itakayoongozwa na Waziri Mkuu, na kuwajumuisha
mawaziri wote wanaohusiana na mashindano hayo, ili kulifanikisha jukumu la
Shirikisho la soka.
Sobhi pia amesema hafla ya ufunguzi na
mechi ya kwanza vitafanyika kwenye uwanja wa taifa wa Cairo wenye uwezo wa
kuchukua mashabiki 74,000, ambao ulifanyiwa matengenezo kabla Misri haijawa
mwenyeji wa michuano ya mwaka 2006.
Waziri mkuu wa Misri, Moustafa Madbouli
amesema mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba tayari wameanza kuurekebisha uwanja
huo, huku rais wa shirikisho la soka Hany Abou Rida akisema wana imani
watashinda kombe hilo. "kuandaa mashindano hayo katika miezi mitatu au
minne ni ishara nzuri ya imani kutoka kwa rais wa FIFA Infantino, na wenzangu
katika CAF. Misri ilipata kura 16 dhidi ya moja kumaanisha wengi wana Imani
kuhusu Misri na uchumi wake.
Wiki iliyopita, Misri ilichukua nafasi
hiyo ya kuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka huu wa 2019 baada ya Cameroon
kunyang'anywa zabuni kutokana na kucheleweshwa kwa ujenzi wa miundombinu na
hali tete ya kisiasa.
Comments