Nyumba kubwa ya kitamaduni
iliyofunguliwa mnamo Oktoba 10, 1988, ni mbadala kwa Nyumba ya Opera ya Khediwe
iliyojengwa na Khedive Ismail mwaka wa 1869 na kuchomwa moto tarehe 28 Oktoba
1971 baada ya kuwa na mnara la kitamaduni kwa miaka 102.
Tareeh ya ujenzi wa nyumba ya kale ya opera inarejea kipindi
cha mafanikio yaliyoshuhudiwa na Khedive
Ismail katika nyanja zote. Khedive Ismail aliamuru ujenzi wa Nyumba ya Opera ya
Khedive katika Mtaa ya Azbekiya huko kati kati ya mji Kairo katika mnasaba wa
ufunguzi wa Mfereji wa Suez , ambapo aliamua kuuitia idadi kubwa ya wafalme wa
Ulaya. Opera ilijengwa katika miezi sita tu , ambapo wahandisi wawili wa Italia
Avoscan na Ross waliweka ramani yake. Khedive Ismael alitaka kuwa opera ya
Misri ishuhudi ufunguzi wa Nyumba ya Opera ya Khedive, ni opera ya Aida .Muziki
wake uliwekwa na mwanamuziki wa Kiitaliano Verdi ,Lakini mazingira yaliwazuia
kuutolewa kwenye ufunguzi wa sherehe, basi Opera ya Rigoletto ilitangulia
wakati wa ufunguzi rasmi , ambao ulihudhuriwa na Khedive Ismail, malikia
Eugenie, mke wa Napoleon III, Mfalme wa Austria na mwana wa mfalme wa Prussia.
Nyumba ya Opera ya Khedive, iliyochomwa asubuhi mnamo Oktoba
28, 1971, Inaweza kubeba hadi watu 850, kuna mahali mahsusi kwa watu muhimu
sana (VIP) Nyumba hiyo ilikuwa na utukufu ya kifahari.
ujenzi
taasisi la Ushirikiano wa Kimataifa la Kijapani (JICA)
liratibitisha na Wizara ya Utamaduni wa Misri huko Kairo, zilikubaliwa kuwa
ramani itafanana na majengo yaliyo kariburamani ilikuwa na sifa za ramani
za kisasa za Kiislamu .
Eneo la ujenzi linajumuisha mita za
mraba 22,772, wakati jengo yenyewe iko kwenye eneo la mita za mraba 13855, na
urefu wa juu wa mita 42.
Katika mwezi wa Machi 1985, ramani iliyochukua mwaka na nusu
ilikamilika na fadhili ilikuwa kwa
juhudi za mikono ya Misri kwa kushirikiana na kampuni ya Kajima kwa ajili ya
kukamilika Mjengo mkubwa katika siku 31 Machi, 1988, baada ya miezi 34 tangu
mwanzo wa kazi ili kuwa alama za karibuni za kitamaduni za Kairo.
Mnamo Oktoba 1988, nyumba hiyo ilifunguliwa mbele ya Rais wa
zamani Hosni Mubarak, Na Amiri Tomohito Auf Mikasa, ndugu mdogo wa Mfalme wa
Japani . Japani pia walishiriki kwa mara ya kwanza katika Misri, ulimwengu wa
Kiarabu na Afrika katika ufunguzi wa jengo hili la kitamaduni , kwa Utendaji wa bendi ya Kabuki, ambayo
inajumuisha wanachama hamsini, Pamoja na wasanii wa cheo cha juu katika uwanja
wa muziki, opera na bale. hivyo jengo hili kubwa lilipatikana tena.ili Misri
iwe nchi ya kwanza katika eneo kujenga nyumba ya opera mara mbili katika muongo
mmoja.
Opera ya sasa ina maonyesho 3: kubwalina viti 1200 , ndogo
lina viti 500, wazi lina viti 600, opera hiyo ilikuwa na jukumu muhimu sana
katika kuimarisha harakati ya sanaa katika Misri. Ambapo inajumuisha:
Bendi la bale la kairo , simfoni, bendi ya Taifa ya Muziki wa
Kiarabu na timu ya ngoma ya kisasa ya ukumbusho .
Opera hutoa saluni za kitamaduni, maonyesho ya sanaa na
sherehe ya muziki.Jumatano, Aprili 25,
sherehe ya kwanza ya Opera ya Misri ilifanyika katika Kituo cha
Utamaduni cha mfalme Fahad huko Riyad chini ya ulilinzi wa Waziri wa Utamaduni
wa Saudi na Misri .
Matawi ya Nyumba ya Opera :
Nyumba ya Opera ya Alexandria.
Nyumba ya Opera ya Damanhour.
Nyumba ya Opera ya Luxor.
Nyumba ya Opera ya Mansoura
Comments