Waziri mkuu anapokea marais wawili wa shirikisho la kimataifa na shirikisho la Kiafrika la mpira wa mikono
- 2019-10-07 13:41:56
Dokta Mostafa Madbuli, Waziri mkuu amepokea Dokta Hassan Mostafa, mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono na Mansour Arymu, mwenyekiti wa shirikisho la Kiafrika la mpira wa mikono.
Dokta Ashraf Sobhy,
Waziri wa vijana na michezo amehudhuria mkutano pamoja na Mhandisi Hesham
Hatab, mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki ya Kimisri na Hesham Nasr, mwenyekiti
wa shirikisho la Kimisri Ia mpira wa mikono.
Wakati wa mkutano,
Waziri wa vijana na michezo, mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa na Waziri mkuu wamejadili mambo yanayohusiana na
kuweka jiwe la msingi la makao mapya ya shirikisho la mpira wa mikono na
kusaini mkataba wa kukaribisha kombe la dunia la mpira wa mikono la wanaume
2021 litakalofanyika nchini Misri.
Dokta Hassan
Mostafa ameashiria imani yake kuwa Misri itaandaa michuano ya dunia ya kiwango
cha juu, akiashiria kuwa kinachoshuhudiwa kwa mpira wa mikono kutoka ongezeko
la umaarufu wake ulimwenguni, ambapo idadi ya wafuasi wa michuano ya dunia ya
mwisho inayokaribishwa kwa Ujerumani imefikia bilioni moja na milioni mia sita,
na iliyoangaziwa katika vituo zaidi ya 190.
Kwa upande wake,
Dokta Mostafa Madbuli amesisitiza kuwa Misri inafanya juhudi zake ili kuandaa
michuano ya kipekee imesifiwa na kuheshimiwa kwa ulimwengu, akiashiria kuwa mafanikio
yanayohakikishwa kwa Misri katika uandaaji wa michuano ya kombe la mataifa ya
Kiafrika ya mpira wa miguu, Madbuli amesifu juhudi zinazofanywa na Dokta Hassan
Mostafa katika uongozi wa mchezo wa mpira wa mikono kwenye kiwango cha dunia,
na jinsi anaiwakilisha Misri katika vikao vya michezo vya kimataifai.
Comments