Mawaziri wa Michezo na Uhamiaji na Gavana wa Sinai kusini wanazindua sherehe ya kwanza ya sharm el sheikh ya Ngamia

waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy  na balozi Nabila Makram waziri wa Uhamiaji , Meja Jenerali Khaled Fouda Gavana wa Sinai kusini na pia Meja Mkuu Jenerali Mohamed El zamlout Gavana wa El wadi al Gadid alifungua sherehe ya kimataifa ya mbio za ngamia za sharmel sheikh kwa kuhudhuria wajumbe wa kiarabu na kiafrika na kundi la wageni waliozuru Sharm El sheikh na wakilishi wa makabila yote ya kiarabu wanaoshiriki katika sherehe  hii , ambapo sherehe hii inakuja kwenye hafla ya kumbukumbu ya miaka 46 ya Misri ya ushindi mtakatifu wa Oktoba

Ngamia 600 wa miaka tofauti kutoka kusini na kaskazini mwa Sinai na Ismalia, Sharqia , Suez , mikoa ya juu ya Misri , Fayoum na El wadi El Gadidi walishiriki kwenye sherehe , shughuli hizo zitaendelea hadi jioni ya oktoba 6

sherehe hii ni mchezo wa kwanza wa ngamia kwa msimu wa michezo wa 2019 / 2020 , imewekwa katika uwanja wa kimataifa ya ngamia imeandaliwa na mkoa wa Sinai kwa kushirikiana na Uongozi  wa vijana na michezo inayoongezwa na Mohamed Fathi

 waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy alikaribisha wageni na ndugu wa Misri kutoka nchi mbalimbali za kiarabu ambayo inatuunganisha pamoja katika maadhimisho na hafla kadhaa alimshukuru Meja Jenerali Khaled Fouda Gavana wa Sinai kusini kwa juhudi zake kubwa katika kuandaa sherehe hii kubwa la kimataifa  inayoonyesha uwezo wa mkoa katika kuvutia matukio kadhaa za michezo za kimataifa

waziri wa michezo alisema kwamba Misri  hujitahidi kuunga mkono nyanja zote hasa uwanja wa michezo ambayo ina udhamini maalum kutoka utawala wa kisiasa , aliongeza kuwa Misri  imekuwa makao makuu wa vyama vya kimataifa vya michezo katika kuandaa matukio makubwa ya kimataifa

-Sobhy alihitimisha matamshi yake kwa kupongeza uongozi wa kisiasa kwenye maadhimisho ya Ushindi wa vita tukufu ya Oktoba , alisema kwamba nchi ya Misri  imepata ushindi na kuvuka mpya tangu mapinduzi ya juni 30 ambayo ilifanya Misri  kuandika historia mpya ambayo ulimwengu wote hutaambia

-kwa upande wake Gavana wa Sinai kusini alisema kuwa leo ni harusi ya kitaifa na kiarabu na mkusanyiko wa makabila yote kwenye ardhi ya Sharm El Sheikh mji wa amani alishukuru Muungano wa  ngamia ya UAE kwa sherehe hii kwa ushirikiano na msaada wake katika kuhamisha ujuzi

Gavana wa Sinai kusini aliashiria umakini mkubwa uliyopewa na nchi iliyopewa na nchi iliyowakilishwa na wizara ya vijana na michezo inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy kwenye sherehe hii ilianza kudhibitisha uwepo wake   ndani na kiarabu

Meja Jenerali Khaled Fouda alielezea kwamba mbio za ngamia ni mchezo muhimu ambao hufanyika kwenye uwanja wa kimataifa ambao una viwango vyote vya mashidano ya kimataifa , umati wa karibu milioni 25 wa mashabiki na mashabiki wa mchezo huo huzunguka ulimwengu wa kiarabu na nchi nyingine  za ulaya

mwisho wa hotuba yake Gavana wa Sinai kusini alisema kuwa uwanja wa mbio wa ngamia ulijengwa kama klabu bora kwa gharama ya paundi milioni 100 na paundi milioni 75 ni msaada wa kibinafsi na ushiriki wa asasi za kijamii kuvutia waarabu na wageni  na wale wanaovutiwa na shughuli za urithi wa kiarabu

hafla ya ufunguzi ilishuhudia maandamano ya ngamia ,Beiskeli na vipindi tofauti vya kisanii , timu ya Sinai kaskazini kiliwasilisha picha kadhaa za kitamaduni za kisanii pamoja na nyimbo kutoka kwa urithi wa sinai uliowasilishwa na msanii Gharib Moamen na pia timu ya Isimailia iliwasilisha vifungu kadhaa vya kisanii na nyimbo nyingi na uchoraji kwa toni za kifaa cha ufuta

jumuiya ya ngamia ya UAE imetoa abiria wenye magari 20 kutoka kwa jumla ya madereva 100 kama zawadi kwa uwanja wa ngamia huko Sharm El Sheikh

Comments