Misri na Huawei hujadiliana kuhamisha teknolojia ya 5G ..na kuitumiwa katika mashindano ya mataifa ya Afrika

Dkt.Mustafa Madbouli waziri mkuu alikutana  jumapili 21/4 na Bwana "Lee Ji" naibu wa rais wa kampuni ya kimataifa ya Huawei na Rubinson Tsao mkuu wa kikanda wa kampuni kaskazini mwa Afrika ,  ambapo Vicent Suna mwenyekiti wa Huawei nchini Misri na  Dkt Amr Talat waziri wa mawasiliano walihudhuria .

wakati wa mkutano huo waziri mkuu  amesifia kiwango cha ushirikiano wa sasa kati ya Misri na China, hasa katika kipindi hivi karibuni, amabapo Rrais wa Misri Abdulfatah El-sisi anatia umuhimu mkubwa ili Misri ifidike  kutoka majaribu ya kimaendeleo na uzoefu za kichina.

Waziri Mkuu aliashiria umuhimu wa uwekezaji wa Huawei katika hali hiyo ya ushirikiano kwa ajili ya kuimarisha uwekezaji wake nchini Misri , hasa katika uwanja wa  teknolojia ya smart miji na nyanja nyingine ambazo Misri inazipa umuhimu zaidi.

kwa upande wake makamu wa rais wa huawei amesisitiza umuhimu wa kampuni kwa  soko za kimisri pamoja na kuchangia kwake kwa ajili ya kuimarisha Nyanja za  maendeleo nchini Misri, akiashiria  kuwa kampuni hupa umuhimu zaidi nyanja za mafunzo kwa ajili ya kujenga vizazi vya waongozi wenye mafunzo na ujuzi duniani kote.

Pia akisisitiza utayari wa Huawei kuongeza ushirikiano yake kwa  ajili ya kusaidia juhudi za serikali na sekta binafsi katika nyanja zote za maendeleo ya kiteknolojia.

Dkt. Amr Talaat waziri wa mawasiliano alisisitiza umuhimu zaidi wa Misri kwa ushirikiano na Huawei katika uwanja wa bandia akili ya kiteknolojia na kuhamisha teknolojia 5G, akibainisha kuwa kampuni itatumika majaribio ya kwanza ya teknolojia hii katika uwanja wa kairo wakati wa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika

Comments