Ujumbe wa Afrika Kusini unafika mjini Kairo ili kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya kitaifa ya Misri ya Olimpiki
- 2019-10-09 20:55:19
Ujumbe wa timu ya kitaifa ya Afrika Kusini ya Olimpiki umefika Kairo katika maandalizi ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya kitaifa ya Misri ya Olimpiki chini ya uongozi wa Shawky Ghareeb, katika siku mbili za 11 na 13 za mwezi wa Oktoba katika uwanja wa mpira wa Kairo.
Shawky Ghareeb
ametangaza majina ya wachezaji 28 kwa kambi inayofanyika sasa kwa ajili ya
maandalizi kwa mechi mbili hizo, na wachezaji hawa ni
Kipa : Omar Radwan,
Omar Salah, Mohamed Sobhy na Mostafa Shobeer.
Watetezi : Osama
Galal, Mahmoud Maraay, Mahmoud Algazar, Ahmed Ramadhani, Mohamed Abd Alsalam,
Mohamed Sadek, Ahmed Abo Alfotooh, Ahmed Ayman na Kareem Aleraky.
Wachezaji wa kiungo
wa kati : Akram Tawfek, Ghbam Mohamed, Amar Hamdy, Naser Maher, Ahmed Hamdy,
Fawzy Alhenawy, Ramadhan Sobhy, Taher Mohamed Taher, Emam Ashor, Abd Alrahman
Magdy na Wageeh Abd Alhaleem.
Washambuliaji :
Mostafa Mohamed, Salah Mohsen, Ahmed Yasser Rayan, Nasser Mansy.
Inatajwa kuwa kura
imewekwa Misri katika kundi la kwanza la kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya
miaka 23, pamoja na timu za kitaifa za ( Mali, Ghana na Cameron)
Comments