Mgombea mmisri kwa jina la Mtu wa Kiafrika wa Mwaka

Hassan Ghazali, mwanzilishi wa Ofisi ya Afrika katika Wizara ya Vijana na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Afrika, amechaguliwa kwa Jumuiya ya Wanasiasa na Viongozi Vijana kuteua Watu wa Mwaka kwa jina la Mtu wa Mwaka miongoni mwa viongozi kadhaa wenye ufanisi katika mabara yote mawili. na hayo yote kulingana na mafanikio yake kama kiongozi mchanga katika hatua za vijana wa Kiafrika na vyanzo vya kienyeji katika ngazi ya kitaifa, kikanda na bara; pamoja na shughuli zake katika kujenga uwezo wa vijana wa Kiafrika na kusaidia Ajenda ya Kiafrika ya 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Kwa jambo hilo , Ofisi ya Vijana ya Kiafrika inawaita kupiga kura na kuunga mkono Mratibu Mkuu na Mwanzishi wa Ofisi ya Vijana ya Afrika Bwana Hassan Ghazali ili kupata lakabu ya Mtu wa mwaka.

Katika muktadha huu, Ghazali atagombea jina hilo pamoja na wagombea watano, hasa Aya Tunbbi wa Tunisia, mjumbe wa Umoja wa Afrika kwa vijana, na mwanariadha mchanga Kastar Seminia kutoka Afrika Kusini.

Tuzo hizo, zilizowasilishwa na Mtandao wa Vijana Wanasiasa na Viongozi, zinalenga kutambua mafanikio ya wabadilishaji waafrika ili kuwatia moyo kwa kuwapa nafasi ya kupata uzoefu muhimu na kuthaminiwa vizuri kwa matarajio yao ya kitaifa na kimataifa na ubora , wakati ambapo wagombea hushindana kwa tuzo kadhaa nazo ni kama : Msanii wa mwaka - Mjasiriamali wa mwaka- Kiongozi wa siku za usoni kwa mwaka- Mwanamke mwanasiasa kwa mwaka- Mwanamume mwanasiasa kwa mwaka- Muundaji wa siasa kwa mwaka- na Mhusika wa mwaka. Tuzo hizo zitawasilishwa wakati wa Mkutano wa Ghana wa kuhudhuria Mkutano wa Vijana wa Viongozi wa Afrika 2019.

Mshindi ataainishwa na kupiga kura ya moja kwa moja kwenye Tovuti ya kilele cha kiafrika kwa viongozi Vijana wa Kiafrika (http://yalsummit.org/vote) Upigaji kura utafungiwa Oktoba 15, wakati ambapo hadi sasa jumla ya kura 4,230 za tuzo ya Mtu wa Mwaka.

Jinsi ya Kupiga Kura:

1. Bonyeza linki hii (http://yalsummit.org/vote)

2. elekea chini kwa kitengo cha "Mtu wa Mwaka", bonyeza "Hassan Ali Ghazaly"

angalia : ukikuta kwamba tovuti haifanyi kazi au haikuwepo basi haya kwa sababu ya wengi wanaopiga kura ndani yake , jaribu kupata tovuti baadaye.


Tunangoja msaada wenu na usaidizi wenu , na ukimpigia kura mgombea wetu, tafadhali basi ushiriki maandishi ya utangazaji na utaratibu wa kupiga kura kwenye kurasa zako za mitandao ya kijamii.

Comments