Chini ya Uangalifu wa Waziri wa Vijana .. Misri inakaribisha kongamano la Shirikisho la Kimataifa la Wanasheria wa Mpira wa miguu
- 2019-10-15 11:52:24
Kwa mara ya kwanza barani Afrika, Misri inakaribisha kongamano la 7 la Shirikisho la Kimataifa la Wanasheria wa Mpira wa Miguu chini ya ushauri wa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo. linalojadili sheria muhimu zaidi za shirikisho la kimataifa kwa mpira wa miguu "FIFA" na masuala magumu khasa barani Afrika na Mashariki ya kati.
Mshauri Nasr Azzam, mwanasheria wa kimataifa ,mtaalamu wa
kesi za usuluhishi wa michezo, alithibitisha kwamba kongamano hilo litafanyika Sanjari na mwenyeji wa Misri na
mafanikio yake ya kupendeza katika kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019, na
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikubali kudhamini mkutano huo
kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa ndani
na nje ya bara la Afrika. , Pia kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Barani Afrika, Tawi la mahakama ya Michezo ya Kimataifa, Kituo cha
Usuluhishi wa Biashara ya Kimataifa barani Afrika na Kituo cha Kimataifa cha
Mafunzo ya Michezo.
Azzam aliashiria kuwa kongamano hilo litajadili kanuni
muhimu zaidi za Shirikisho la Soka la Kimataifa, hasa kanuni mpya ya FIFA, juu
ya hali na uhamishaji wa wachezaji na marekebisho muhimu zaidi na msimamo wa
mawakala wa wachezaji chini ya kanuni mpya, pamoja na kujadili haki za
utangazaji katika mpira wa miguu katika kiwango cha kimataifa na kikanda.
Aliongeza kuwa mkutano huo ni fursa kwa wadau wote wa mpira
wa miguu wanaovutiwa na sheria na kanuni za mpira wa miguu, iwe washiriki wa
vyama, vilabu au wanasheria kujadili wataalam wakubwa ulimwenguni katika eneo
hili, ambapo kongamano hilo litafasiriwa
kutoka Kiingereza kwa Kiarabu na Kifaransa. na usajili utapatikana
wazi hadi Oktoba 15.
Wakilishi wa mashirika makubwa ya kimataifa ya mpira wa
miguu kama vile Mario Galafotti (Mkurugenzi wa Kamati Zinazojitegemea za FIFA),
Omar Ongaro (Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Soka ya FIFA), Erica Montemor
Ferreira (Mkuu wa Mchezaji wa FIFA), na nyota wa mpira wa miguu Mchezaji wa
Mpira wa Miguu wa Misri Ahmed Hossam Mido, Anthony Bafoe, Naibu Katibu Mkuu wa
CAF, Mustafa Abdulla, Meneja Ushirikiano wa CAF, Ashta Mahamat Saleh, Meneja
Masuala ya Sheria wa CAF, Meneja Masoko wa Uuzaji wa CAF, Dan De Young, Mkuu wa
Idara ya Sheria ya Michezo (ECA) ).Alexandaria Gomez Bruinwood (Mshauri wa
Sheria kwa FIFPro), Dokta Ismail Selim . Abdullah El Shehaby ( Mwanasheria -
Misri ), Abdullah Shehata ( Mwanasheria - Misri ) na mwakilishi Misri LA LIGA
PRO MEDIA.
Comments