waziri wa vijana na michezo akihudhuria semina ya mazungumzo ya vijana kuhusu ushindi mtakatifu wa Oktoba mkoani wa Suez

 waziri wa vijana na michezo Dokta  Ashraf Sobhy na gavana wa Suez , Meja Jenerali Abdel Majid Sakr walikutana na kikundi cha vijana wa kiume na wa kike kutoka mkoa wa Suez katika semina ya majadiliano iliyofanyika klabu ya Al nasr petroli huko Suez

kongamano hilo lilikuja juu ya ushindi wa vita vya Oktoba chini ya kichwa cha  "  tunaisherehekea kwa Misri yetu tunahisi fahari  kwa jeshi yetu na tunajivunia kwa  ushindi wetu " mbele ya Meja Jenerali Mustafa Abdel Latif na Meja Jenerali Yosri Amara , mahojiano hayo  yalikuwa chini ya kichwa cha mkutano wa vijana wa Suez

kongamano hilo lilishughulikia mashindano ya wanajeshi wa Misri wakati ushindi wa vita vya Oktoba mnamo 1973 , na uwezo wa kumshinda adui na kurejesha kiburi na kufanikisha ushindi kwa Misri

 waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy alisema kwamba vijana wa wamisri ndio nguvu halisi , kwamba lazima tujue na kwenda mahali pake pa asili , katika ujenzi na maendeleo kwa ajili ya Misri

 waziri wa vijana na michezo alisisitiza jukumu la vijana wa wamisri katika kufanikisha maendeleo ya nchi katika nyanja mbali mbali aliongeza kuwa wizara inafanya kazi ili kusaidia uwezo wa vijana na kukuza ujuzi wao kupitia programu na miradi inayotekelezwa katika mikoa yote kwa mwaka mzima

waziri huyo alisema juu ya juhudi zilizowekwa katika maendeleo ya makazi ya vijana na michezo na kufuata utendaji wao , kuongeza shughuli na mipango ili vijana waweze kufanya mazoezi ya shughuli mbalimbali

 Dokta Ashraf Sobhy amepongeza vijana wamisri na watu wa Misri kwenye siku ya kumbukumbu ya ushindi  Mtakatifu wa vita vya  Oktoba , alisifu jukumu la wanajeshi na polisi katika kudumisha usalama wa Misri na kupambana na kuondoa ugaidi mweusi

Comments