Vijana na Michezo : washindi watatu kutoka nchi za Afrika kwa Tuzo ya Ubora kwa Vijana waandishi wa habari na waandishi wa vyombo vya habari"

 Wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika na kusambamba na Uandaaji wa Michuano ya mataifa ya kiafrika 2019 ,Bibi Adaa Waranga toka Kenya alipata cheo cha kwanza katika uwanja wa Vyombo vya habari vya kiafrika kutoka tuzo ya Ubora kwa vijana waandishi wa habari na waandishi wa vyombo vya habari, pia Bwana Ledevid Oko kutoka Nigeria alipata nafasi ya pili, wakati ambapo Bwana Labudy Omar kutoka Algeria alipata nafasi ya tatu.

 

Hayo yote yalitokea baada ya Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy aliidhinisha tija za tuzo ya Ubora kwa vijana waandishi wa habari na vyombo vya habari katika uwanja wa Vijana na Michezo, iliyotolewa kwa mara yake ya kwanza kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa vijana waandishi wa habari na vyombo vya habari chini ya umri wa miaka 40, nayo ilijumuisha viwanja kadhaa navyo ni kama Uandishi wa habari wa kimichezo, Uandishi wa habari wa Vijana, Picha ya kimichezo bora zaidi, Vyombo vya habari vya Runinga, Mtangazaji bora zaidi, na hivyo inaamuliwa kwamba kila mshindi atapata tuzo bora ya kifedha pamoja na Oscar ya mashindano kulingana na sheria ya tuzo.

 

Pia inatarajiwa kutangaza tuzo zinazohusu jambo hilo wakati wa sherehe rasmi inayoainishwa hivi karibuni, wakati ambapo kamati kuu kwa mashindano iliamua kutoa tuzo fulani kwa mmoja wa wachambuzi wa kimichezo wakubwa, tuzo inayobeba jina la mwandishi adhimu aliyekufa Nagib Elmestekawy, na tuzo nyingine kwa Mtangazaji mmoja wa kimichezo, inayobeba jina la Mtangazaji mkubwa aliyekufa Fayez Elzomor, pamoja na Heshima kubwa na ya pekee kwa wanachama wa kamati za waamizi.




Comments