Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amekutana leo na Hisham El Tohamy, mwenyekiti wa Shirikisho la mpira wa vinyoya ili kuangalia mipango yote ya mwisho ya kukaribisha Misri kushindana katika toleo la tano la Mashindano ya Kimataifa ya mpira wa vinyoya ya Misri ambayo yatafanyika chini ya uangalizi wa Wizara ya Vijana na Michezo katika kipindi cha kuanzia tarehe 17 hadi 20 Oktoba 2019 katika ukumbi uliyofunikwa wenye namba 4 katika Uwanja wa Kimataifa wa Kairo.
Mashindano hayo ni
pamoja na wachezaji 126 wanaowakilisha nchi 31, pamoja na wachezaji 79 wa
Kimisri na wachezaji 47 kutoka nchi tofauti za ulimwengu iliyoshiriki katika
mashindano hayo.
Sherehe ya
kuhitimu mashindano hayo itafanyika
Jumapili ijayo katika ukumbi uliofunikwa namba 4 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa
Kairo mbele ya kikundi cha wanariadha na wanahabari, bodi ya Shirikisho la
mpira wa vinyoya ya Misri na wakilishi wa Wizara ya Vijana na Michezo.
Comments