Kuanza shughuli za wiki ya vijana wa vyuo vikuu vya Kiafrika huko Aswan

 Chini ya uangalizi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, rais wa jamhuri, Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi itazindua shughuli za Wiki ya Vijana ya Vyuo Vikuu vya kwanza 2019, iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Aswan chini ya uangalizi wa Dokta  Ahmed Ghallab, Rais wa Chuo Kikuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Juu ya Wiki hiyo. Mnamo kipindi cha Oktoba 19-25 , Uwanja wa Michezo wa Aswan.

 

Wiki ya Vijana ya Vyuo vikuu vya Afrika inakusudia kuimarisha  ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya Kiafrika, kuhimiza mazungumzo ya kitamaduni miongoni mwa wanafunzi wa Kiafrika, kuanzisha mtandao mwenye habari na umoja wa habari kwa viongozi wa vijana barani Afrika, na kubadilishana tamaduni kati ya vyuo vikuu vikuu vya Afrika, na kubadilishana utamaduni Kati ya vijana wa vyeo vikuu vya kiafrika, kupitia ujumuishaji wa taasisi za elimu ya juu barani Afrika kupitia michezo. Timu za kitamaduni, kubadilishana uzoefu na kuenea kwa umoja.

 

Imepangwa kuwa nchi ishirini na moja za Kiafrika, pamoja na Nigeria, Sudani, Chad, Camerun, Cote de lvoire, Afrika ya Kati na Tanzania, na vyuo vikuu 22 vya Misri vitashiriki katika hafla za wiki hiyo.

 

Ni muhimu kutaja kuwa wiki ya kwanza ya vijana wa vyuo vikuu vya Kiafrika ni tukio la kitaifa ambapo watu bora wa vijana wa vyuo vikuu vya Kiafrika hukutana katika aina mbali mbali za shughuli za kitamaduni, kisanii na michezo, inayojumuisha shirika la mashindano mengi ya michezo na kitamaduni na mipango ya kijamii. 

Comments