Kairo inashuhudia tukio la sherehe ya Hitimisho ya wanafunzi wa Sudan kwenye vyuo vikuu vya kimisri

Jukwaa la Wizara ya vijana na michezo lilishuhudia sherehe ya Hitimisho ya Wanafunzi wa Sudan kwenye Jamhuri ya kiarabu ya Misri , kudi cha 19, iliyofanyikwa kwa Wizara pamoja na ushirikiano wa " Idara kuu kwa programu za kiutamaduni na kijitolea na Ofisi ya vijana waafrika" kwa uongozi kwa Dokta Ashraf Sobhy kwa kushirikiana na Jumuia ya kiafrika.

Dokta Amany El Taweel " Mkurugenzi wa programu ya kiafrika kwenye kituo cha Al Ahram ka masomo ya kisiasa na kimikakati" , Dokta Amna Fazaa " Rais wa klabu ya mwanamke mwafarika", Balozi Muhamed Nasr El Din ' Rais wa Jumuia ya kiafrika" Dokta Sayed Rashad ' Mratibu mkuu wa masuala ya wanafuzi waafrika kwenye chuo kikuu cha Kairo" Bwana Khalil Mamnoon ' Mwandishi na mtafiti", na Bwana Hassan Ghazaly " Mwanzishi wa ofisi ya kiafrika na naibu wa rais wa shirikisho la vijana waafrika" wao wote walihudhuria sherehe ile.

na hayo yote yalikuja wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika 2019, na kuunganisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi mbili, pamoja na kuunga mkono Ajenda ya Afrika 2063, malengo ya maendeleo endelevu na Mkataba wa vijana waafrika unaosisitiza kupatikana nafasi za kuonyesha maoni kwa vijana waafrika.

Sherehe ilikusanya maonyesho kadhaa ya kuimba na kikale kwa nchi ndugu ya Sudan, baadaye kuheshima wahusika wakubwa katika suala la kiafrika, miongoni mwao Dokta Amna Fazaa " Rais wa klabu ya mwanamke mwaafrika" , Mwandishi Khalil Manoon, Dokta Mohamed Ali Nofal " Mkuu wa kitivo cha masomo ya kiafrika" Kapteni Abd El Moniem Shata " Mtaalamu wa Mpira kwenye Umoja wa kiafrika" na Bwana Hassan Ghazaly " Mwanzishi wa Ofisi ya kiafrika, na Naibu wa rais wa shirikisho la vijana waafrika".


na Sherehe ilihitimishwa kwa kuwaheshima kundi la 19 la wanafuzi wa Sudan kwenye Vyuo vikuu vya kimisri.

Comments